JIMMY IGOHE ANENA KUTOKA NEW YORK KUHUSU MAANDALIZI YA OLIMPIKI

Viwanja vya Olimpiki ya Tokyo 2020
  
 Waheshimiwa,

Jamani habari ndio hiyo sasa !!!

Tokyo wataandaa michezo ya 2020 Olympics.
     
Niliposikia hivyo niliuma vidole nikamwaza mwanamichezo wetu wa zamani Bwana JUMA IKANGAA alivyokuwa akipata vifaa vya ASICS na jinsi alivyoiinua kampuni hii miaka ya nyuma. Kushiriki kwakeTokyo, Fukuoka, Boston na New York City Marathons na kuwatangaza ASICS na kuwa kampuni kubwa inayoheshimika kwa sasa, na pia yeye binasfi bado anapewa vifaa vya ASICS mpaka leo hii.
    
    Suala sasa ni kuwa je, anaubavu wa kuwashaiwishi ASICS watumwagie vifaa kwa ajili ya wanamichezo wetu?  Hali ya kusikitisha imeonekana kwenye mashindano ya taifa huko Morogoro ambapo wachezaji wetu walionekana kuwa na moyo lakini ni vitendea kazi (vifaa) hawana.
    
    Juma Ikangaa amekuwa mgumu wa kusaidia kupata vifaa kwa ajili ya wachezaji kwani alishafanya hivyo 1984 na kuangushwa, na hivi karibuni alijaribu tena lakini kulikuwa na masharti kadhaa. Hivyo ni jukumu la RT pamoja na TOC kuongea naye ili kuona kama mambo yatafanikiwa.
    
    Mimi niko tayari kusaidia kama nilivyofanya huko nyuma na kampuni ya FILA, kama RT watalipa usafiri, BROOKS na FILA wako kusaidia kutoa vifaa kwa ajili ya wachezaji wetu kwa ajili ya mashindano ya taifa ya 2014 ambayo nahisi yatakuwa kabla michezo ya COMMMONWEALTH GAMES huko Glasgow, UK.
    
    Tujaribu kukimbia maana wenzetu wako mbali kweli,
    
    Jimmy

Comments

Popular

GIDABUDAY KUHAMASISHA UJENZI WA KIJIJI CHA MICHEZO TANZANIA LENYE JINA YA MWANARIADHA MKONGWE BW.JOHN STEPHEN AKHWARI

Rio Olympics: Brazil win men's volleyball gold, GB's Joyce takes boxing silver – as it happened

Olympics 2016: Usain Bolt completes sprint double, Jade Jones retains taekwondo title

Rio Olympics: Swimmer Lochte apologises for 'robbery' saga