Baraza jipya la mawaziri: Safari hii rais Kikwete aamua kutumia subira yake mwenyewe, hamna presha, atatangaza wakati wowote

Dr. Mwakyembe & Dr. Magufuli
Watanzania wanasubiria kwa hamu kuona majina ya mawaziri watakaoteuliwa kumalizia ungwe ya uongozi wa awamu ya nne chini ya uongozi wa Mh.Jakaya Kikwete.

Hata hivyo safari hii imekuwa tofauti kwani rais Kikwete ameamua kuumiliki uteuzi wake bila presha wala kuvuja kwa siri kabla ya siku yenyewe.

Watanzania hata hivyo wanayo imani kubwa kwamba rais atawateua watu wenye uzalendo na upendo kwa nchi yao, tofauti na mawaziri wengi walioshuhudiwa wakitumia nyadhifa zao vibaya kwa kutoa lugha korofi na zenye hadaa.

Taarifa za kuaminika zinabainisha kwamba "ugali tayari ila twasubiri ipoe kabla ya kuliwa". Muda wowote tutapata kujua nani yupo ama nani hayupo katika "Magic list of honorees" 

Taarifa hiyo imeongeza kuwa "Dr. John Magufuli na Dr. Harison Mwakyembe ni kati ya mawaziri wasiokuwa na shaka wala homa katika kipindi hiki kigumu kama mawaziri wengine" 

Wanajifahamu kwamba ni wachapa kazi wazuri na lazima watarudi barazani bila wasiwasi. Endelea kufuatilia habari hapa hapa!

Comments

Popular

GIDABUDAY KUHAMASISHA UJENZI WA KIJIJI CHA MICHEZO TANZANIA LENYE JINA YA MWANARIADHA MKONGWE BW.JOHN STEPHEN AKHWARI

Rio Olympics: Brazil win men's volleyball gold, GB's Joyce takes boxing silver – as it happened

Olympics 2016: Usain Bolt completes sprint double, Jade Jones retains taekwondo title

Rio Olympics: Swimmer Lochte apologises for 'robbery' saga