Latest News

Friday, January 24, 2014

MAZISHI: Charles Kyando maarufu kwa jina la Tola kuzikwa siku ya Jumamosi tarehe 25/01/2014Mazishi ya aliyekuwa kocha wa mchezo wa tenisi Charles Kyando maarufu kwa jina la Tola yatafanyika kesho nyumbani kwake Mwananyamala kwa Ali Maua.

Marehemu alifariki usiku wa kuamkia jana baada ya kuugua kwa muda mfupi. Mazishi hayo yatafanyika kesho kwa mujibu wa habari kutoka kwa familia ya marehemu.

“Huu ni msiba kwa chama cha Tennis Tanzania na taifa kwa ujumla; pengo lake kamwe halitazibika” alisema kocha wa tenis mwenzake ndg Hassan Kassim.

‘Mwnyezi mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi amina’ Pole nyingi kwa familia, ndugu na marafiki bila kusahau Tanzania Tennis Association.

No comments:

Post a Comment