Msiba chama cha Tennis: TTA yapata msiba mzito baada ya kocha wake mkongwe CHARLES KYANDO (TOLA) kufariki ghafla

Charles Kyando (Tola) Enzi za uhai wake



Sekta ya michezo Tanzania imepata msiba mkubwa usiku wa kuamkia leo kwa kufiwa na Charles Kyando maarufu kwa jina la Tola, Kyando alifariki ghafla baada ya kuugua kwa muda mfupi.


Charles Kyando (Tola) alizaliwa 1968 jijini Dar Es Salaam na wakati wa uhai wake aliwahi kucheza mashindano mbalimbali ya mchezo wa tenisi na kufikia viwango vya kitaifa kati ya miaka ya 1980 hadi 1990.

Baada ya kustaafu kama mchezaji bwana Kyando alikuwa kocha wa mchezo wa tenisi na pia alikuwa mtaalam maarufu wa kusuka rakets za mchezo huo.


Marehemu ameacha mjane na watoto wawili, pia marehemu ameacha pengo kubwa na isiyozibika katika mchezo wa tenisi na katika chama cha tenisi Tanzania (Tanzania Tennis Association).


Kuhusu taratibu za mazishi na taarifa zozote kuhusiana na msiba huu tafadhali endelea kusoma blogu hii ya Utaifa Kwanza.

Comments

Popular

GIDABUDAY KUHAMASISHA UJENZI WA KIJIJI CHA MICHEZO TANZANIA LENYE JINA YA MWANARIADHA MKONGWE BW.JOHN STEPHEN AKHWARI

Rio Olympics: Brazil win men's volleyball gold, GB's Joyce takes boxing silver – as it happened

Olympics 2016: Usain Bolt completes sprint double, Jade Jones retains taekwondo title

Rio Olympics: Swimmer Lochte apologises for 'robbery' saga