Mwandishi wa BBC Ann Waithera afariki: Shirika la habari la BBC limempoteza mwandishi wa habari Ann Waithera

Ann Waithera enzi za uhai wake

Ann alikuwa anafanya kazi na BBC katika ofisi za Nairobi na amekuwa akiugua Saratani ya Ubongo kwa karibu miaka miwili.

Ann aliwahi kuwa ripota wa BBC mjini Addis Ababa Ethiopia. Kabla ya kujiunga na BBC Ann alifanya kazi na shirika la habari la Nation Media Group nchini Kenya na Citizen TV. Ann alikuwa na umri wa miaka 39.
Waandishi wenza wa Ann BBC wameelezea watakavyomkumbuka Ann katika enzi zake alipokuwa anafanya kazi nao.

Razvan Scortea mmoja wa wakuu wa BBC amesema : "Nimeshtushwa sana na kifo cha Ann. Alikuwa mtu mzuri , mwerevu mpenda watu na mwenye matumaini kwa kila jambo. Mungu ambariki.''

Mkuu wa BBC Afrika Solomon Mugera ameelezea kuwa ni jambo la kuhuzunisha sana kumpoteza Ann.
''Nimehuzinika sana. Anne alikuwa mwandishi mahiri . Kila nilipomtembelea nilivutiwa sana na matumaini ya Ann kupona. Hata katika mkesha wa krismasi, nilipozungumza na Ann alikuwa mcheshi sana. Nakumbuka Ann ndiye alikuwa mwandishi wetu wa kwanza mwenye uwezo wa kuripoti katika lugha zaidi ya moja mjini Addis Ababa Ethiopia,'' alisema Solomon

Mkuu wa idhaa ya kiswahili ya BBC Ali Saleh naye pia ameelezea kushtushwa kwake na kifo cha Ann akimkumbuka kama mwandishi mahiri na mwenye kujitolea kwa kazi zake.

'Nakumbuka kufanya naye kazi kabla ya yeye kwenda Addis Ababa, na kufanya mipango ya kila alichotarajiwa kufanya. Matumaini mengi ila yamekatizwa mapema mno.'' alisema Elizabeth Blunt aliyekuwa mwandishi wa BBC mjini Addis Ababa kabla ya Ann kuchukua usukani kutoka kwake. 

"Anne alikuwa mmoja wa waandishi mahiri wa BBC nchini Kenya . Kifo kimetupokonya mmoja wa waandishi wenye talanta kuu Afrika Mashariki.'' Kauli ya David Okwemba mhariri mkuu wa ofisi ya BBC Nairobi Kenya.

Mhariri mkuu wa idhaa ya Hausa mjini London Mansur Liman, ametuma rambi rambi kwa familia ya Ann, akiwaombea utulivu wakati huu mgumu. 

Chanzo: BBC SWAHILI                                  

Comments

Popular

GIDABUDAY KUHAMASISHA UJENZI WA KIJIJI CHA MICHEZO TANZANIA LENYE JINA YA MWANARIADHA MKONGWE BW.JOHN STEPHEN AKHWARI

Rio Olympics: Brazil win men's volleyball gold, GB's Joyce takes boxing silver – as it happened

Olympics 2016: Usain Bolt completes sprint double, Jade Jones retains taekwondo title

Rio Olympics: Swimmer Lochte apologises for 'robbery' saga