Rais Mheshimiwa Dkt Jakaya Kikwete amefanya uteuzi wa makatibu tawala wa mikoa mitano na kuwahamisha makatibu tawala wengine na wakurugenzi wa majiji


Sipora J. Liana

Makatibu tawala wapya ni ndugu Wamoja A.Dickolangwa anayeenda mkowa wa Iringa ambako alikuwa kaimu katibu tawala wa mkoa. 

Ndugu Abdallah D.Chikota anayeenda Lindi kabla alikuwa mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Newala, ndugu Symthies E.Pangisa anayeenda mkoa wa Rukwa kabla alikuwa kaimu katibu tawala wa mkoa wa Mtwara, ndugu Alfred C.Luanda aliyeteuliwa kuwa katibu tawala mkoa wa Mtwara kabla alikuwa mkurugenzi wa halmashauri ya manispaa ya Tabora. 

Pia dugu Jackson L.Saitabau anakwenda mkoa wa Njombe kabla alikuwa katibu tawala msaidizi wa mkoa wa Arusha.

Waliohamishwa ni pamoja na Beatha Swai kutoka katibu tawala mkoa wa Pwani kwenda ofisi ya waziri mkuu TAMISEMI, pia yupo ndugu Sipora J.Liana kutoka mkurugenzi wa jiji la Arusha kwenda ofisi ya waziri mkuu TAMISEMI na ndugu Benedict ole Kuyan kutoka katibu tawala mkoa wa Tanga kwenda katibu tawala mkoa wa Mara.

Wengine ni ndugu Salum M.Chima kutoka katibu tawala Rukwa kwenda Tanga na Ndugu Mgeni Baruani kutoka katibu tawala mkoa wa Njombe kwenda katibu tawala mkoa wa Pwani.

Wengine ni ndugu Juma R. Idd kutoka mkurugenzi wa jiji la Mbeya na kuwa mkurugenzi wa jiji la Arusha, Eng.Omar Chambo aliyekuwa katibu mkuu wizara ya uchukuzi amehamishiwa mkoa wa Manyara kama katibu tawala wa mkoa na Dkt John Ndunguru aliyekuwa naibu katibu mkuu wa wizara ya ujenzi anahamishiwa mkoa wa Kigoma kama katibu tawala wa mkoa huo.

"Bila shaka leo tendawili la uteuzi wa mawaziri utapata majibu" habari zimenukuliwa sehemu!

Comments

Popular

GIDABUDAY KUHAMASISHA UJENZI WA KIJIJI CHA MICHEZO TANZANIA LENYE JINA YA MWANARIADHA MKONGWE BW.JOHN STEPHEN AKHWARI

Rio Olympics: Brazil win men's volleyball gold, GB's Joyce takes boxing silver – as it happened

Olympics 2016: Usain Bolt completes sprint double, Jade Jones retains taekwondo title

Rio Olympics: Swimmer Lochte apologises for 'robbery' saga