Latest News

Tuesday, February 4, 2014

Kikwete: Wajumbe Bunge la Katiba kutangazwa leo, keshoRais Jakaya Kikwete amesema uteuzi wa majina 201 ya wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba umekamilika na kati ya leo na kesho, atayatangaza pamoja na tarehe ya kuanza kwa Bunge hilo.

Bunge la Katiba litakalokuwa na wajumbe 640, litakutana kwa siku 90 kujadili Rasimu ya Katiba iliyotolewa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Desemba 30, mwaka jana.

“Bunge la Katiba litakutana katika wiki ya tatu ya mwezi huu. Mambo yanayosubiriwa ni mawili tu, uteuzi wa wajumbe 201 na siku ya kuanza kwa Bunge hili. Mambo haya yote ninayesubiriwa kuyakamilisha ni mimi tu,” alisema Rais Kikwete alipokuwa akihutubia katika kilele cha maadhimisho ya miaka 37 ya kuzaliwa kwa CCM.

Alisema kazi ya uteuzi wa wajumbe hao ilikamilika tangu juzi na kinachofanyika sasa ni kuhariri majina hayo na kurekebisha mambo kadhaa.

“Jumatatu (leo) tutayapitia majina haya ili tuone kama tunaweza kurekebisha. Baada ya hapo tutaweza kutangaza na inaweza kuwa siku hiyohiyo au kesho yake (Jumanne), hazitazidi siku hizi mbili,” alisema.
Alisema hivi sasa ukarabati katika Ukumbi wa Bunge, Dodoma bado unaendelea na mkandarasi ameeleza kwamba hadi Februari 10, mwaka huu atakuwa amemaliza kazi.

CHANZO: Mwananchi

No comments:

Post a Comment