Sports Diplomacy: Waziri Membe kupeleka wanariadha 40 nje ya nchi

Mhe. Bernard Membe
Tanzania inaelekea kupata nafasi ya kupeleka timu ya riadha nchini China, Ethiopia na Uturuki kwa maandalizi ya kuwanoa vijana kwa mashindano ya madola na kwa msaada wa waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Bernard Membe.

RT imeonyesha dalili za kuchagua wanariadha mezani badala ya mashindano ya wazi ili kufanya mchujo wa kidemokrasia. 

Mfumo ambao nchi za wenzetu kama Kenya wanafanya ili kuepusha upendeleo wa aina yoyote. Katibu wa RT Sulemain Nyambui amekaririwa na vyombo vya habari akidai kupeleka majina kwa waziri Membe.

'Wazalendo na wapenda haki tunadhani ipo haja ya kuandaliwa mashindano maalum yatakayopewa viwango kadha ambayo wakimbiaji wakifikia ndio wachaguliwe kwa uwazi badala ya kumpa mwanya kiongozi  moja kumpendelea ndugu ama jamaa yake'

Kuna tetesi kwamba kuna vijana na makocha ambao wamehakikishiwa safari hizo kwa ahadi maalum kwamba wakijiandaa kutoa chochote watahakikishiwa wanasafiri bila kujali uwezo wao.

Tunashauri makocha wote waitwe wapewe interview wajieleze na wakifaulu ndio waende! 

Kama ambavyo mtu hawezi kwenda Olympics bila kwanza kufikia viwango! Wanariadha pia wapewe mtihani huru wa kushindana kwanza na watakaoshinda waende kutuwakilisha.


'Waziri Bernard Membe kama unapenda haki basi usipokee majina ya kuchaguliwa mezani bali hakikisha kunawekwa mashindano ya kuchagua timu kwa uwazi nawe pia uhakikishe kwamba haki ya kidemokrasia inatendeka'

Comments

Popular

GIDABUDAY KUHAMASISHA UJENZI WA KIJIJI CHA MICHEZO TANZANIA LENYE JINA YA MWANARIADHA MKONGWE BW.JOHN STEPHEN AKHWARI

Rio Olympics: Brazil win men's volleyball gold, GB's Joyce takes boxing silver – as it happened

Olympics 2016: Usain Bolt completes sprint double, Jade Jones retains taekwondo title

Rio Olympics: Swimmer Lochte apologises for 'robbery' saga