Tanzania Tennis Association kuadhimisha Siku ya tenisi duniani


M/Kiti wa TTA Methusela Mbajo / katikati

Jumamosi wiki hii (March 1st) chama cha tenisi Tanzania (TTA) kitaungana na vyama vya tenisi duniani pamoja na wadau kusherehekea siku ya tenisi ulimwenguni.

Maadhimisho hayo yatafanyika katika viwanja vya Dar Es Salaam Gymkhana Club ambapo maadhimisho yataambatana na mafunzo ya bure kwa watoto na wakubwa watakaopenda kujifunza mchezo wa tenisi.

Shughuli zitaanza saa tatu asubuhi hadi saa nane mchana, mafunzo yataendeshwa na makocha waliobobea wa tenisi wakiwemo  Kiango Kipingu na Hassan Kassim.

Watanzania mnakaribishwa kiingilio ni bure, ‘njoo uangalie, njoo ujifunze, njoo ufurahi’

Comments

Popular

GIDABUDAY KUHAMASISHA UJENZI WA KIJIJI CHA MICHEZO TANZANIA LENYE JINA YA MWANARIADHA MKONGWE BW.JOHN STEPHEN AKHWARI

Rio Olympics: Brazil win men's volleyball gold, GB's Joyce takes boxing silver – as it happened

Olympics 2016: Usain Bolt completes sprint double, Jade Jones retains taekwondo title

Rio Olympics: Swimmer Lochte apologises for 'robbery' saga