Latest News

Monday, March 24, 2014

KATIBA MPYA: Wafugaji wahofu Katiba kutowatambua


KUNDI la wafugaji nchini wameeleza hofu ya maisha yao kutokana na rasimu ya pili ya Katiba kutokuwa na vipengele vinavyotambua uhalali wao wa kuishi na shughuli wanazofanya.

Akizungumza na Tanzania Daima juzi, Mwakilishi wa wafugaji ambaye ni mjumbe wa Bunge Maalumu la Katiba, Makeresia Jibubu, alisema baada ya kupitia rasimu hiyo wamebaini kuwepo na vipengele ambavyo havijaonyesha thamani ya wafugaji nchini.

Alisema katika rasimu hiyo wafugaji wametajwa katika kipengele cha malengo makuu na sera ya nchi na kusema ili suala la wafugaji liwe na umhimu linapaswa liwekwe kwenye kipengele cha wajibu na haki za binadamu, ili waweze kutambulika kisheria.

CHANZO: Tanzania Daima

No comments:

Post a Comment