Latest News

Friday, March 21, 2014

KAZI KWENU WABUNGE: JK aweka wazi faida na changamoto za serikali tatu


Marais wetu wakifurahia jambo
Katika Hotuba yake iliyofuatiliwa na wengi katika historia ya utazamaji wa televisheni, rais Kikwete ameonyesha kutoegemea upande wowote japo alikiri kuwa na haki ya kutoa mawazo yake.


Wengi wamefurahia uthubutu wake wa kutoegemea upande wowote japo kwa mbali sana hisia zake ziliweza kudhihirika. Amesisitiza “Maridhiano” ndio itakayowapatia watanzania katiba bora.


Hata hivyo makofi yaliweza kusikika kwa wingi kila alipoweza kuelezea changamoto za muundo wa serikali tatu; kitendo kinachoashiria kwamba wanaopenda serikali mbili wapo wa kutosha japokuwa bila maridhiano hawataweza kupata ‘Absolute Majority” vivyo hivyo hata wale waumini wa serikali tatu nao watahitaji ‘Political Compromise’ 


Mtazamo wangu: 'Katiba mpya inakuja' japo kutakuwepo na ‘Turbulence and rough ride ahead’ Wabunge wote waliopo Dodoma ni watanzania wenzetu,wenye masilahi sawa na sisi, wenye uzalendo na wenye kujitambua! 

Hivyo tuwaombe waanze kazi kwa kujali masilahi ya taifa la leo na lile taifa la kesho.

No comments:

Post a Comment