MOTISHA KWA WANAMICHEZO: Tuzo wanamichezo bora Juni 27




TUZO za wanamichezo bora Tanzania 2013/14 zinatarajiwa kutolewa jijini Dar es Salaam Juni 27 zikiwa na kaulimbiu ya ‘Wanamichezo Tupige Vita Ujangili’.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jana na Mwenyekiti wa kamati ya tuzo hizo, Rehure Nyaulawa, walikutana Dar es Salaam juzi na kukubaliana masuala mbalimbali juu ya kuboresha tuzo hizo ikiwemo tarehe ya kuzitoa.

Nyaulawa alisema ukumbi utatangazwa kwa ushirikiano wa kamati hiyo pamoja na Kamati ya Utendaji ya Taswa na tayari juhudi za pamoja za kuzungumza na wadhamini mbalimbali wakubwa na wadogo kwa nia ya kufanikisha tuzo hizo katika tarehe iliyopangwa yameanza na kuna muelekeo mzuri.

CHANZO: Tanzania Daima

Comments

Popular

GIDABUDAY KUHAMASISHA UJENZI WA KIJIJI CHA MICHEZO TANZANIA LENYE JINA YA MWANARIADHA MKONGWE BW.JOHN STEPHEN AKHWARI

Rio Olympics: Brazil win men's volleyball gold, GB's Joyce takes boxing silver – as it happened

Olympics 2016: Usain Bolt completes sprint double, Jade Jones retains taekwondo title

Rio Olympics: Swimmer Lochte apologises for 'robbery' saga