Training Center: Tanzania inahitaji kituo kikukwa cha michezo yote

Zambia Olympic Youth Development Center
 Mwaka 2004 Tanzania ilipata bahati ya kuahidiwa kujengewa kituo kikubwa cha kisasa cha michezo (Tanzania Olympic Youth Development Center) ambayo ingegharimu USD 10million lakini viongozi wa TOC kwa kushirikiana na viongozi wasio wazalendo walikwamisha.

Kilichotakiwa na IOC ni kuhakikishiwa kwamba eneo kubwa lisilo na utata wa kisheria linapatikana ikiwa na vithibitisho vya kiumiliki ili hapo baadaye kusiwepo na utata (contradiction) za kisheria.

Bila aibu wala uzalendo kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC) ilihakikisha kwamba kituo hicho hakijengwi kwa sababu ya wao kuhofia masilahi yao ya upatikanaji wa tenda za kimichezo katika center zao walizojiwekezea.

Kwa mfano:  kama mtu anapata tenda ya Copa Coca-Cola ya Tsh: Bilioni kila mwaka alafu atawezaje kupata kiasi hicho cha pesa iwapo taifa litakuwa na center yake? Hivyo kigogo mmoja tu mwenye center yake alishawishi kamati nzima waikatae ofa hiyo ya IOC nao kwa akili zao ndogo wakaafiki upuuzi huo.


Hatimaye TOC ikashindwa kurudisha majibu kwa IOC ndipo IOC ikaamua kupeleka ofa hiyo Zambia na wazambia hawakuchezea nafasi hiyo na hivi sasa kuna kituo kinachoitwa Zambia Olympic Youth Development Center.

Je wizara na baraza la michezo (BMT) wamefanya juhudi gani kuwachukulia hatua watu hao?  Watu ambao kimsingi ni ‘Wahujumu Uchumi’ maana kupindisha (Divert) masilahi ya taifa ni kuhujumu uchumi wa taifa kwani watoto wengi wenye vipaji wangenufaika na kituo hicho bila gharama.

'Tutaendeleza mapambano ya mapinduzi ya kimichezo hadi pamba za masikio ya waheshimiwa serikalini zidodonke na waanze kusikia vilio vyetu'

Comments

Popular

GIDABUDAY KUHAMASISHA UJENZI WA KIJIJI CHA MICHEZO TANZANIA LENYE JINA YA MWANARIADHA MKONGWE BW.JOHN STEPHEN AKHWARI

Rio Olympics: Brazil win men's volleyball gold, GB's Joyce takes boxing silver – as it happened

Olympics 2016: Usain Bolt completes sprint double, Jade Jones retains taekwondo title

Rio Olympics: Swimmer Lochte apologises for 'robbery' saga