UTAIFA KWANZA: Holili yadhamini Sokoine Mini Marathon

KLABU ya Holili Youth Athletic Club (HYAC) ya mjini Holili, mkoani Kilimanjaro, imejitosa kudhamini mbio za Sokoine Mini Marathon zinazotarajiwa kufanyika Aprili 12, mwaka huu katika Kijiji cha Monduli Juu, Wilaya ya Monduli, mkoani Arusha.

Katika udhamini huo, HYAC imetoa sh milioni moja zitakazotumika kuchapisha namba (Bibs), 1,000 za utambulisho za wanariadha.

Akizungumza na Tanzania Daima jana, Mkurugenzi wa HYAC, Domician Genandi, alisema kilichomsukuma kufanya hivyo ni moyo wa uanamichezo na kuongeza kuwa, kwa mwaka huu wamedhamiria kuongeza nguvu zote kuinua mchezo wa Riadha nchini.

“Nimeamua kusaidia nikiwa kama mdau, sababu lengo letu ni kuendeleza michezo Tanzania, sisi wadau tunatakiwa tuwe na mtazamo wa ushindi kama taifa na si ushindi wa klabu zetu binafsi tu, au wanariadha wetu tu, HYAC tunatambua jitihada binafsi zinazofanywa na waandaaji kumuenzi hayati Sokoine,” alisema Genandi.

Aidha, Genandi alisema kwa mwaka huu klabu yake inatarajiwa kushirikisha wanariadha wengi zaidi, ambako lengo lake ni kuhakikisha anaendeleza rekodi ya mwaka jana.

Kwa upande wake, Mratibu wa mbio hizo, Wilhelm Gidabuday alisema kwa udhamini huo HYAC inakuwa klabu ya kwanza ya riadha hapa nchini kudhamini mashindano yanayoandaliwa na wadau wengine wa riadha na kuongeza kuwa, katika hilo wameonesha kweli kwamba wana nia nzuri ya kuendeleza michezo hapa nchini hasa riadha.

CHANZO: Tanzania Daima

Comments

Popular

GIDABUDAY KUHAMASISHA UJENZI WA KIJIJI CHA MICHEZO TANZANIA LENYE JINA YA MWANARIADHA MKONGWE BW.JOHN STEPHEN AKHWARI

Rio Olympics: Brazil win men's volleyball gold, GB's Joyce takes boxing silver – as it happened

Olympics 2016: Usain Bolt completes sprint double, Jade Jones retains taekwondo title

Rio Olympics: Swimmer Lochte apologises for 'robbery' saga