‘Jakaya Kikwete Sports Village’ kujengwa Dom

Mfano wa ramani ya Center inayotarajiwa ya Dr. Jakaya Kikwete National Sports Village
MAANDALIZI ya ujenzi wa kijiji cha michezo kitakachojulikana kama Jakaya Kikwete Sports Village yanaendelea vizuri, ambako tayari Ikulu, Baraza la Michezo la Taifa (BMT) na Wizara ya Michezo wametoa baraka kijengwe mjini Dodoma.
Akizungumza na Tanzania Daima, Mratibu wa ujenzi wa kituo hicho, Wilhelm Gidabuday, alisema ujenzi wa kituo hicho kikubwa na cha kwanza nchini, tayari maandalizi yake yameshafikia pazuri na Ikulu ya Tanzania kupitia ofisi ya Katibu wa Rais, imeshawapa baraka ya kutumia jina la Rais katika kituo hicho.
Gidabuday alisema, wiki iliyopita walikutana na Katibu wa Rais, ambako waliwasilisha maombi yao na kukubaliwa na kwamba, kuanzia sasa kituo hicho ambacho ujenzi wake utasaidia kuinua vipaji vya michezo yote hapa nchini, kitafahamika kama kituo cha michezo cha Jakaya Kikwete (Jakaya Kikwete Sports Village).
“Nidokeze tu kuwa, mipango yote inakwenda sawa, tumeshafikisha ujumbe wetu Ikulu na imekubalika, awali tulipanga kituo chetu tukiite John Steven Akhwari Sports Village, lakini baada ya kukaa na Mzee Akhwari, kwa pamoja tuliridhia kituo hiki kitumike kama sehemu ya kumpa heshima
Rais wetu, Ndugu Jakaya Mrisho Kikwete, hivyo kitafahamika kama Jakaya Kikwete Sports Village,” alisema Gidabuday.
Gidabuday ambaye pia anaratibu mbio za Kumbukumbu ya miaka 30 ya kifo cha Sokoine, Sokoine Mini Marathon, pamoja na matembezi ya amani kutoka Ujiji – Kigoma mpaka Dar es Salaam, alisema wamepanga kutumia shughuli zote mbili kuwafahamisha wananchi kuhusu umuhimu wa ujenzi wa kituo hicho katika maendeleo ya sekta ya michezo na utamaduni hapa nchini.
Wakati huo huo, waandaaji wa msimu wa pili wa Sokoine Mini Marathon, zitakazofanyika Kijiji cha Monduli Juu, wametangaza rasmi sehemu ambako fomu za ushiriki wa mbio hizo zitapatikana.
Akizungumza na waandishi wa habari, Mratibu wa Mbio hizo, Wilhelm Gidabuday, alisema, fomu za ushiriki wa mbio hizo kwa mwaka huu zitapatikana wilayani Monduli, katika Kijiji cha Monduli Juu.
CHANZO: Tanzania Daima


Comments

Popular

GIDABUDAY KUHAMASISHA UJENZI WA KIJIJI CHA MICHEZO TANZANIA LENYE JINA YA MWANARIADHA MKONGWE BW.JOHN STEPHEN AKHWARI

Rio Olympics: Brazil win men's volleyball gold, GB's Joyce takes boxing silver – as it happened

Olympics 2016: Usain Bolt completes sprint double, Jade Jones retains taekwondo title

Rio Olympics: Swimmer Lochte apologises for 'robbery' saga