Latest News

Wednesday, April 30, 2014

SARA RAMADHANI atuhumiwakutumia dawa za kuongeza nguvu


Hivi karibuni imeripotiwa na magazeti ya Tanzania kwamba Sara Ramadhani amefungiwa na Chama Cha Riadha Duniani (IAAF) kwa kipindi cha miaka miwili asishiriki mashindano ya kitaifa na kimataifa.

Mshangao zaidi ni pale gazeti moja la kila siku liliporipoti kwamba ameefungiwa maisha! Bila shaka mwandishi aliyechapisha habari hizo hana uchunguzi wowote kuhusu sheria za IAAF.

Kwa uchunguzi wangu nimetambua kwamba ni kweli shutuma hizo zipo na kwamba adhabu iliyotolewa ni ya miaka miwili tu kulingana na sheria za IAAF, na kwamba mtuhumiwa anayo nafasi ya kujitetea kwa kukata rufaa maana inawezekana akawa ametumia dawa asizofahamu kwani ilishawahi kutokea.

2004 Bernard Lagat wa Kenya (ambaye kwa sasa ni raia wa Marekani) alituhumiwa na kupewa adhabu kama ya Sara Ramadhani lakini baada ya yeye na kocha wake kutoa maelezo ikabainika kwamba alitumia dawa za kawaida ambazo wakati wa vipimo ilionekana damu yake ina caffeine nyingi.

Muda mfupi baadaye adhabu yake ikafutwa! Hivyo basi ni bora tukasubiri rufaa ya dada yetu huyo kabla ya kushabikia adhabu ambayo huenda ikafutwa!

No comments:

Post a Comment