Latest News

Thursday, July 10, 2014

Angela Kairuki: Atakayevunja rekodi riadha taifa mil. 1/-

NAIBU Waziri wa Sheria na Katiba, Angela Kairuki, ameahidi zawadi ya shilingi milioni moja kwa atakayevunja rekodi katika mashindano ya riadha ya taifa yatakayofanyika Juni 12 na 13, jijiji Dar es Salaam.


Ahadi hiyo ilitolewa jana na naibu waziri huyo wakati akifunga semina ya waamuzi 22 watakaoendesha mashindano hayo na kuongeza kuwa wanariadha wanahitaji sapoti waweze kufanya vizuri kitaifa na kimataifa.

“Michezo inakuza uchumi, pia ni sehemu ya maisha ya binadamu, ni muhimu tukiwa tunawapa sapoti wanariadha mbalimbali, hivyo mimi kama mdau wa mchezo huo naahidi kutoa hela hiyo ili aendelee kuwa mwanariadha bora,” alisema.


Alisema serikali itaendelea kuwasaidia wanamichezo katika mipango yao ili kurudisha heshima ya nchi kwa wanariadha wake kufanya vizuri kama ilivyokuwa kwa Filbert Bayi, Suleimani Nyambui na wengineo.


Mwenyekiti wa Chama cha Riadha Mkoa wa Dar es Salaam (DAA), Zainabu Mbiro, alisema waamuzi walioshiriki seminda hiyo ni kutoka mikoa mbalimbali ikiwa na lengo la kukuza mchezo huo.


“Kawaida Mkoa mwenyeji unatakiwa kuandaa waamuzi wa mashindano ya taifa, baada ya kupewa nafasi ya kuendesha mashindano hayo sisi kama mkoa tulilazimika kuendesha mafunzo hayo ambayo tuliwakutanisha waamuzi kutoka mikoa mbalimbali ili kuweka sawa na kukuza mchezo huu,” alisema.


Alisema semina hiyo ilikuwa ya wiki moja na ilikuwa inaendeshwa katika Uwanja wa Taifa huku cheti kwa washiriki kikitambulika kitaifa.


CHANZO: Tanzania DaimaNo comments:

Post a Comment