Latest News

Friday, July 11, 2014

MSIBA MKUBWA: Mwili wa Saria kuagwa leo

MWILI wa aliyekuwa mwanariadha, kocha na kiongozi wa zamani wa Riadha Tanzania (RT), Ernest Saria aliyefariki usiku wa kuamkia Jumanne, unatarajiwa kuagwa leo saa 3 asubuhi katika kituo cha Polisi, Kurasini jijini Dar es Salaam.

Akithibitisha hilo jijini Dar es Salaam jana, Katibu Mkuu wa RT, Suleima Nyambui alisema, shughuli za kuagwa kwa mwili wa marehemu, zitaanza saa tatu asubuhi katika kituo hicho kabla ya kusafirishwa kupelekwa mjini Moshi, Mkoani Kilimanjaro.


Saria alifikwa na umauti huo akiwa nyumbani kwake, Pugu jijini Dar es Salaam, bada ya kuugua maradhi ya malaria na dengue.


Katika uhai wake, Saria aliwahi kushika nyadhifa mbalimbali katika mchezo wa RT ikiwemo ya Katibu wa Kamati ya Ufundi ya RT na Mjumbe wa Kamati ya Utendaji hadi mwaka juzi, alipowania nafasi ya Makamu wa Pili wa Mwenyekiti Ufundi.


Aidha, wakati wa ujana wake aliwahi kuwa bingwa wa mbio za meta 400 na 800 nchini na kuipeperusha nchi katika mashindano mbalimbali ya kimataifa na kufanya vizuri, hivyo kifo chake kimeacha pengo kubwa katika tasnia ya michezo.

CHANZO: Tanzania Daima


No comments:

Post a Comment