Ikangaa apigiwa debe ‘kumrithi’ Malinzi uenyekiti wa BMT

Col. Rt. Juma Ikangaa
Mwanariadha wa zamani , Juma Ikangaa anatajwa kurithi nafasi ya uenyekiti  wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) baada ya Dioniz Malinzi kumaliza muda wake wa miaka mitatu juzi Jumapili.

 Habari za ndani ambazo gazeti hili ilizipata zilieleza kuwa kati ya majina yaliyopendekezwa na Serikali, Ikangaa anapewa nafasi kubwa ya kuchukua mikoba ya Malinzi.

 “Yalipendekezwa majina kadhaa ya watu maarufu ambao Serikali iliona wanastahili kuongoza BMT baada ya Malinzi kumaliza muda wake na Ikangaa ndiye anapewa nafasi kubwa ya kuwa mwenyekiti,” kilisema chanzo chetu.

 Mwenyewe (Ikangaa) alipotafutwa na gazeti hili kujua msimamo wake, hakukubali wala kukataa kutaka cheo hicho zaidi ya kueleza hana taarifa zozote juu ya uteuzi huo.

Gazeti hili lilimtafuta, Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Profesa Elisante Ole Gabriel ili kujua ukweli wa habari hizo lakini ambaye hakuwa tayari kulizungumzia suala hilo.

 “Niko kwenye kikao, suala la Ikangaa kuchaguliwa kuwa mwenyekiti wa BMT siwezi kulizungumzia labda uwatafute wenyewe BMT waseme,” alisema Profesa Ole Gabriel kwa kifupi.

CHANZO: Mwananchi

Comments

Popular

GIDABUDAY KUHAMASISHA UJENZI WA KIJIJI CHA MICHEZO TANZANIA LENYE JINA YA MWANARIADHA MKONGWE BW.JOHN STEPHEN AKHWARI

Rio Olympics: Brazil win men's volleyball gold, GB's Joyce takes boxing silver – as it happened

Olympics 2016: Usain Bolt completes sprint double, Jade Jones retains taekwondo title

Rio Olympics: Swimmer Lochte apologises for 'robbery' saga