Baraza la Mawaziri Kenya labadilishwa

Rais Uhuru Kenyatta
Rais wa Kenya amefanya mabadiliko katika Baraza lake la Mawaziri na kuwaacha wote ambao wizara zao zilikumbwa na tuhuma za ufisadi.

Rais Uhuru Kenyatta amechukua hatua hiyo siku moja tu baada ya kutangaza ufisadi kuwa tishio kwa usalama wa kitaifa. Rais ameahidi kufanya mabadiliko zaidi katika afisi yake hivi karibuni.

Katika hotuba ilioonyeshwa kwa njia ya Televisheni, Rais Kenyatta ameongeza idadi ya wizara kutoka 16 hadi 20 na kuongeza idara mpya chini ya wizara mbalimbali katika kile alichosema ni kusaidia mawaziri kutekeleza majukumu yao bora zaidi.

Idara hizo zimeongezwa kutoka 26 hadi 41. Rais Kenyatta amefanya mabadiliko katika baraza lake la mawaziri baada ya mawaziri sita kulazimika kujiondoa kutokana na wizara walizosimamia kuhusishwa na ufisadi huku wawili kati yao wakikabiliwa na kesi mahakamani.

Ni mabadiliko yaliyotarajiwa hasa baada ya hatua ya aliyekuwa waziri wa Ugatuzi Anne Waiguru kujihuzulu mwishoni mwa juma kutokana na kile alichosema ni ushauri wa daktari wake- baada ya usumbufu aliopata wizara yake ilipohusishwa na sakata kadhaa za ufisadi.

Kwa mujibu wa katiba idadi ya mawaziri inapaswa kuwa kati ya 14 na 22 na hivyo kujiuzulu kwa Bi Waiguru kulisababisha idadi hiyo kupungua hadi 13. Baraza jipya la mawaziri linajumuisha wanawake wanne na wanaume 16.

Baadhi ya mawaziri wamesalia katika nafasi zao huku wengine wapya wakiteuliwa kuchukua nafasi za mawaziri waliohusishwa na ufisadi. Hatua itakayofuata sasa ni kwa mawaziri wapya kuchunguzwa na kamati ya bunge kabla ya kuidhinishwa kikamilifu.

Serikali ya Rais Uhuru Kenyatta imekuwa ikikabiliwa na changamo ya ufisadi katika wizara kadhaa na kumekuwepo shinikizo sio tu kutoka kwa wananchi lakini pia kutoka kwa mashirika ya kijamii,viongozi wa upinzani na hata mabalozi wa nchi za kigeni kutaka hatua zichukuliwe.

Chanzo: bbcswahili

Comments

Popular

GIDABUDAY KUHAMASISHA UJENZI WA KIJIJI CHA MICHEZO TANZANIA LENYE JINA YA MWANARIADHA MKONGWE BW.JOHN STEPHEN AKHWARI

Rio Olympics: Brazil win men's volleyball gold, GB's Joyce takes boxing silver – as it happened

Olympics 2016: Usain Bolt completes sprint double, Jade Jones retains taekwondo title

Rio Olympics: Swimmer Lochte apologises for 'robbery' saga