Latest News

Thursday, November 19, 2015

Mwanamichezo ateuliwa Waziri Mkuu

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa
Rais John Pombe Magufuli leo amemteua waziri mkuu mpya ambaye amejinadi kama mwanamichezo.


Kassim Majaliwa hii leo ameapishwa kuwa wazii mkuu baada ya kuteuliwa na rais hatimaye kupitishwa na bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwa waziri mkuu mpya wa serikali ya awamu ya tano.


“Mimi ni mwanamichezo, ni kati ya wakufunzi 27 wa TFF, nitamwelekeza rais amteue waziri wa michezo anayefaa kwani michezo itatutangaza kimataifa” Hayo ni baadhi ya maneno yake waziri mkuu mpya.

No comments:

Post a Comment