Latest News

Tuesday, December 1, 2015

Baraza la Mawaziri kusheheni wabunge wa kuteuliwa na Rais

Rais Dr John Pombe Magufuli
Mpaka sasa watu wanasubiri baraza la mawaziri ili kuunda serikali rasmi ya Magufuli.
Vyanzo vya ndani vinasema kuwa Magufuli atateua Mawaziri 18 tu, ambapo kutakuwa na wizara 15 na manaibu waziri wa tatu.

Rais mpaka sasa anaimani na wabunge wachache sana ndani ya ccm ambao hawafiki hata 15.
Habari zinasema kuwa Bado Rais anaendelea na mchakato wakutafuta watu makini katika taasisi za serikali ambao wengi wao hawatozidi umri wa miaka 40. Watu hao anategemea kuwapa ubunge na kuwateuwa kuwa mawaziri.

Mpaka sasa Rais ananafasi 9 ya viti hivyo, na inasemekana anateuwa watu nane kuwa wabunge na kupewa wizara nyeti.

Inasemekana hakuna waziri wala naibu wake wa serikali ya Kikwete atakae pata nafasi ya uwaziri au unaibu. Wengi watakuwa ni wabunge wapya na wabunge wa zamani ambao walikuwa msitari wa mbele kuisimamia serikali kutoka CCM.

Moja ya mbunge ambae atapewa wizara ni mbunge toka mkoa wa tabora ambae hakuwa na ukakasi kukemea ufisadi.

Pia inaelezwa kuwa Makam Urais anashinikiza J.Makamba apewe wizara ya mambo ya nje, lkn Magufuli hataki kusikia jina hilo.
Kuhusu Mwigulu, huyu na Magufuli haziendani toka zamani, hivyo msitegemee kabisa.

Rais anataka kuwa na team itakayokuwa tiifu kwake na sio mamluki toka msogaa.


Chanzo: Jamii Forum