Mafisadi Hananag wauza Viwanja, Vyanzo vya Maji

Mt Hanang / Mlima wa tatu Tanzania
Wilaya ya Hanang ina bahati ya kuwa na mlima wa tatu Tanzania (Mt Hanang 3,417m) baada ya (Mt Kilimanjaro 5,895m )na (Mt Meru 4,565m), milima yote mitatu ikiwa kanda ya kaskazini mwa Tanzania.


Mwenyezi mungu ametujalia utajiri wa misitu, wanyama na maji, lakini binadamu wamekuwa mafisadi na wababe, kufikia hatua ya kubadili matumizi ya utajiri huu kwa kutumia mabavu, pesa na rushwa.


Ni miaka mingi hivi sasa tangu serikali ilipoamuru wavamizi wa Bonde la mto Endamanang kuondoka, hata ilani iliwekwa na serikali; lakini kwa sababu ya ulafi wa baadhi ya maofisa wa jeshi la polisi wakishirikiana na viongozi wakuu wa wilaya ya Hanang wasio waaminifu ilani iliharibiwa, hadi leo hii Bonde la Endamanang bado linalimwa na watu kumi tu.


Hawa hapa wanaolima Bonde la mto Endamanang lililopo Nangwa-Hanang kwa kulindwa na polisi wa Hanang;

(1)Nino Yahhi, (2)Sikukuu Axwesso, (3)Damasi Yatosh, (4)Disdery Yatosh,  (5)Izraeli Yatosh, (6)Zakayo Yatosh, (7)Isaya Baha, (8)Xufo Baha, (9)Gelangi Baha & (10)Moshi Hhau


Mbabe aliye uza bonde ni Safari Massay ambaye kwa sasa ni mwenyekiti wa bodi ya maji ya mto Nangwa na mto Endamanang. 

Aliyefanikisha uwakala wa kusambaza hongo kwa viongozi wa wilaya na maofisa wa polisi ni Wema Nade maarufu Wema Kipisi, pia anajiita "OCD wa Nangwa"

DC wa sasa wa Hanang anasubiri nini kuwakamata wahusika?, DC Makonda aliweza kuwakamata maofisa wake kwa kuchelewa, kwa nini hawa waharibifu wasikamatwe?

Picha na habari / Wilhelm Gidabuday








Comments

Popular

GIDABUDAY KUHAMASISHA UJENZI WA KIJIJI CHA MICHEZO TANZANIA LENYE JINA YA MWANARIADHA MKONGWE BW.JOHN STEPHEN AKHWARI

Rio Olympics: Brazil win men's volleyball gold, GB's Joyce takes boxing silver – as it happened

Olympics 2016: Usain Bolt completes sprint double, Jade Jones retains taekwondo title

Rio Olympics: Swimmer Lochte apologises for 'robbery' saga