Latest News

Thursday, December 10, 2015

Rais John Pombe Magufuli ametangaza baraza la Mawaziri leo

Rais John Pombe Magufuli
Leo Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania, Dr John Magufuli anatangaza baraza la mawaziri wa Jamhuri wa jamhuri ya muungano wa Tanzania. Tuwe pamoja kulifahamu baraza letu.

Magufuli: Kumekuwa na speculation nyingi na watanzania wamekuwa na hamu kubwa ya kujua baraza la mawaziri, baada ya kusubira kwa muda mrefu, baada ya kuapa tulitakiwa angalau tarehe kumi tuwe tumetangaza baraza.

Tuliona angalau tujiridhishe kwanza, baraza lililopita lilikuwa na mawaziri na manaibu zaidi ya 59, tukaona tuwe na baraza dogo. Hatuwezi kukaa bila baraza, katika baraza hili, wizara nyingi tumeziunganisha na kutakuwa na wizara 18 na tutakuwa na mawaziri 19 tu, kuna baadhi ya wizara zitakuwa na mawaziri na hazitakuwa na manaibu waziri.

Lengo ni kutimiza ahadi yetu ya kuwa na baraza dogo kupunguza gharama na effective kwa kufanya kazi. Zilitengwa bilioni 2, mawaziri watakapoteuliwa waende semina elezi, baraza nitakaloliteua halitakuwa na semina elekezi na fedha tutaelekeza sehemu nyingine kama ni madawati au kwenye elimu bure. Watafanya semina elekezi wenyewe ndani kwa ndani.

WIZARA
Ofisi ya Rais, Tamisemi, utumishi na utawala bora: Mawaziri ni George Simbachawene na Angela Kairuki, Naibu waziri Jaffo Selemani Said

Ofisi ya makamu wa Rais, muungano na mazingira: Makamba na naibu wake ni Mpina

Ajira, walemavu: Jenista Mhagama, Naibu nimemtua mbunge, Pos Abdallah ambae ni mhadhiri Dodoma

Ulemavu: Waziri ni Anthony Mavunde

Kilimo, mifugo na uvuvi: Waziri ni Mwigulu Lameck Nchemba, Wiliam Nashe naibu waziri

Ujenzi, uchukuzi na mawasiliano: Waziri bado sijamtafuta, naendelea kumfikiria, Naibu waziri Edwin Ngonyani.

Fedha na mipango: Waziri bado tunamtafuta, naibu waziri ni Kijachi

Nishati na madini: Waziri ni Professa Muhongo, Naibu waziri ni Medadi

Katiba na sheria: Waziri Harisson Mwakyembe

Mambo ya nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki: Waziri ni Augustino Mahiga ambae nimemteua kuwa mbunge na kisha waziri, Naibu ni Dr Suzan Kolimba.

Ulinzi na kujenga taifa: Waziri ni Dr. Hussein Mwinyi

Wizara ya mambo ya ndani: Charles Kitwamba

Ardhi na maendeleo ya makazi: Waziri ni Wiliam Lukuvi, Naibu Angelina Mabula

Maliasili na Utalii: Waziri bado, naibu ni Ramo Makala

Viwanda na biashara: Waziri Charles Mwijage

Elimu, Sayansi na ufundi: Waziri bado hajapatikana, Naibu ni Stella Manyanya

Afya, maendeleo ya jamii na Ustawi wa jamii: Ummy Mwalimu, Naibu ni Hamis Andrea Kingwangala

Habari, utamaduni, wasanii na michezo: Nape Nnauye, naibu Anastazia Wambura

Wizara ya maji na umwagiliaji: Makame Mbarawa ambae nilimteua kuwa mbunge, Naibu ni Kamwene
=====================

Swali: Kuna baadhi hukutaja, tatizo ni nini hasa kwa wizara ambazo hujateua? Wabunge wa chama chako hawana sifa? Usimamizi wa baraza unatarajia zitafanya kazi zake Dodoma ukiondoa TAMISEMI?

Magufuli: Nilitegemea ungeniuliza kwanini sikuteua siko niliyoteuliwa, subira yavuta heri, hawa wameanza na wengine watafata. Usiwe na haraka. Kuhusu Dodoma tutatekeleza yaliyoko kwenye ilani ya chama cha mapinduzi.

Swali: Umesema hakutakuwa na semina elekezi, utafanya nini waweze kwenda na kasi ya hapa kazi?

Magufuli: Niliyowachagua wote wana CCM na wengi wao ni wabunge, walinadi ya sera hapa kazi na ndio maana haja ya semina elekezi, spidi ni hiyo hiyo ndio maana hatutatumia semina elekezi ya bilioni mbili.

Manyerere Jackton: Kwa kupunguza ukubwa wa baraza la mawaziri na kwa kulinganisha na tulipotoka, serikali itakuwa imepunguza kiasi gani?

Magufuli: Wewe ndie utapiga hesabu, kwa vile ni mmiliki wa gazeti huwa unapiga hesabu huwa unapata kiasi gani. Utanisaidia katika kupunguza baraza tutakuwa tumesevu kiasi gani na zile tulizosevu za gharama elekezi, kuchelewa kutangaza baraza na wale ambao sijawataja na bahati nzuri nyie waandishi mnaweza kupiga hesabu vizuri. Zipo nchi zina mawaziri wengi mpaka kufikia hata 70, wizara 44, manaibu na mawaziri. Tutakapomaliza tutakuwa na baraza la watu 34 tu.

Wakienda kule mawaziri wakafanye kazi kweli ndio maana sisi tulipochaguliwa tulifanya kazie kweli na hatukwenda kwenye semina elekezi na tulijielekeza, wakajieleze kwenye maeneo yao.

Wasihangaike kufanya sherehe kwa sababu ni kazi ngumu na kama wapo wanaopenda kufanya sherehe wajiandae kufanya sherehe siku wakifukuzwa, contract ni miaka mitano. Wakawafanyie kazi watanzania bila kuwabagua, Baraza hili la wizara 15 tumejiridhisha linaweza kufanya kazi tunayowatarajia kuifanya effectivly. Ngoja tukimaliza uteuzi wote tutajua tumesave kiasi gani ili ziweze kwenda kwa wananchi.

Raymond(Uhai Production): Siku saba zimetimia, wafanyabiashara wamesharesha zile hela?

Magufuli: Swali hilo kamuulize kamshna wa kodi TRA.

SWALI: Kuna wizara ina mawaziri wawili, huko kazi ngumu?

Magufuli: Kafanye utafiti hio wizara imeunganisha wizara ngapi, utapata majibu.

Swali: Katika baraza, kuna mawaziri wa baraza lililopita, ulizangatia nini wakati wa uteuzi?

Magufuli: Umekosea hata kupiga hesabu, Kafanye hesabu vizuri, waliorudi ni saba na sio kumi? Ukipiga utaelewa ni vigezo gani nilivyotumia.

Asanteni sana na ninawashukuru

No comments:

Post a Comment