Latest News

Monday, December 7, 2015

Rais Magufuli amtimua Mkurugenzi, M/Kiti TPA na Katibu Mkuu Miundombinu

Katibu Mkuu (W) Uchukuzi Shaaban Mwinjaka
Rais John P. Magufuli leo amevunja Bodi ya Bandari ya Jijini Dar es Salaam, kutokana na kashfa ya upotevu wa makontena ulioisababishia Serikali hasara ya mabilioni ya Shilingi.

Mbali na kuvunja bodi hiyo, pia ametengua uteuzi wa Mwenyekiti wa Bodi hiyo, Mhandisi Prof. Joseph Msambichaka na kumsimamisha kazi Katibu Mkuu Wizara ya Uchukuzi, Shaaban Mwinjaka.

Maamuzi hayo yametolewa Jijini Dar es Salaam na Waziri Mkuu, Majaliwa Kassim Majaliwa, kwa niaba ya Rais ambapo amenukuliwa na Fikra Pevu akisema maamuzi hayo ya Rais yamekuja muda mfupi baada ya kubaini kasoro nyingi za kiutendaji kwa watumishi hao wa Serikali.

Pamoja na mambo mengine, amesema Rais amewasimamisha kazi maofisa nane kutoka Bandari ya Dar es Salaam baada ya kubainika walihusika kwa namna moja ama nyingine katika sakata hilo.

Kassim Majaliwa amesema kutenguliwa kwa uteuzi huo kunatokana na ziara alizofanya katika Bandari ya Dar es Salaam na kubaini uwepo wa mianya ya ukwepaji kodi ikiwemo ya Makontena 2,387 yaliyopitishwa kati ya Machi na Septemba mwaka jana.

Kwa mujibu wa Waziri Mkuu, mara baada ya agizo hilo, ameagiza wahusika wote wakamatwe na wawekwe chini ya ulinzi ili kusaidia upelelezi ikiwa ni pamoja na kueleza makontena yaliyopotea yalikuwa ya nani na yalikuwa na thamani ya shilingi ngapi.

Watuhumiwa hao watatakiwa kuwezesha makontena hayo yaweze kulipiwa kodi kutokana na awali kutolipiwa kodi. Katika ziara aliyoifanya katika Shirika la Reli Nchini (TRL), Waziri Mkuu alibaini matumizi mabaya ya fedha ya Sh.Bilioni 13 nje ya utaratibu ambao uchunguzi unakamilishwa kwa waliohusika.

Kadhalika, amesema upotevu huo unatokana na mfumo usiokidhi wa kupokelea malipo ambao unatoa mwanya wa kupoteza mapato ya Serikali na kutaka mfumo huo ubadilishe kufikia Desemba 11.

Ameeleza kwamba kutokana na utendaji wa bandari huo mbovu, ripoti iliwataja waliohusika na upitishaji wa makontena hayo na bila ya kuwepo kwa taarifa yeyote, hivyo amewasimamisha kazi wasimamizi 8 wa Bandari Kavu (ICD) ambao ni Happygod Naftari, Juma Zaar, Steven Naftari Mtui, Titi Ligalwike, Lydia Prosper Kimaro, Mkango Alli, John Elisante pamoja na James Kamwomwa.

Wengine ambao hakuwemo kwenye ripoti hiyo ambao ni viongozi wa sekta zilizotoa ruhusa makontena kutoka ndani ya bandari lakini ni wahusika wakuu ni pamoja na Shaban Mngazija, aliyekuwa Meneja Mapato, Rajab Mdoe ambaye ni Mkurugenzi wa Fedha na Mkuu wa Bandari Kavu, Ibin Masoud Kaimu Mkurugenzi wa Fedha, Apolonia Mosha Meneja wa Bandari Msaidizi (Fedha).

Massawe aliteulia na Samwel Sitta kushikila nafasi ya Mhandisi Madeni Kipande aliyesimamishwa kwa tuhuma za utendaji mbovu ili kupisha uchunguzi. Hata hivyo, wakati wa tamko hilo, wahusika wote walikuwa hawapo wakati tamko hilo linatolewa na Waziri Mkuu.No comments:

Post a Comment