Latest News

Saturday, February 20, 2016

Nape amtoa Henri Lihaya kafara, abakiza majipu BMT

Henry Lihaya

Waziri wa Habari, Utamaduni, Wasanii na Michezo Mh. Nape Nnauye February 19 ametembelea Baraza la Michezo Tanzania (BMT) kujua namna ya utendaji wa baraza hilo unavyokwenda pamoja na changamoto zinazowakabili.

Lakini katika ziara hiyo, imeshuhudiwa Katibu Mkuu wa baraza hilo Henry Lihaya aking’olewa kwenye nafasi hiyo ambapo Mh. Nnauye amemwagiza Katibu Mkuu wa Wizara yake amtafutie nafasi nyingine Wiarani.

“Mtendaji mkuu amekaa miaka saba, sasa nadhani inatosha, naagiza katibu mkuu wa wizara ampangie kazi nyingine wizarani kuanzia leo atafanya utaratibu wa kuripoti wizarani kwa katibu mkuu”, amesema Nnauye.

“Halafu kwa mujibu wa sheria ya BMT mwenyekuteuwa mtendaji mkuu ni mwenyekiti wa bodi ambaye nimemwomba alete mapendekezo, sheria inasema atateuwa kwa idhini ya waziri na ndiyo maana nimechukua nafasi ya kuondoka na aliyekuwepo halafu yeye alete mapendekezo mimi nikiridhia atamteuwa ili aje hapa alete chachu mpya”.

“Kwanini tunafanya mabadiliko BMT, ni kwasababu huu ndiyo moyo wa michezo. Tukipabadilisha hapa bila shaka michezo yetu itakwenda vizuri maana hawa ndiyo wanasimamia vyama vya michezo na mtendaji mkuu anakiri kwamba vyama vingi vya michezo havina program za michezo na wenye kusimamia ni hawa”.

“Mtendaji mkuu atakayekuja nitakabananaye koo sana kuhakikisha kwamba anakuwa mkali sana kusimamia program za michezo. Kama hakuna mipango hata usipofanya chochote itaonekana ni sawa tu, lakini ukiwa na mipango unaweza kupima kama utekelezaji unafanyika au haufanyiki kuna maendeleo au hakuna”.

Lengo la ziara hiyo ilikuwa ni kutekeleza agizo la waziri mkuu la kufanya maboresho kwenye baraza hilo ili lieandane na kasi inayotakiwa.

Mh. Nnauye ameahidi kushughulikia changamoto ambazo zinalikabili baraza hilo zikiwemo za fedha, watumishi wachache, matatizo ya sheria na mambo mengine kuhakikisha baraza linaenda sawa.

No comments:

Post a Comment