Latest News

Tuesday, May 24, 2016

Benki ya Azania yadhamini mashindano ya riadha kwa watoto

Mfano wa namba za ushiriki wa AZANIA BANK KIDS RUN zitakazofanyika Juni 5 katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar Es Salaam

Juni 5 mwaka huu Chama Cha Riadha Tanzania RT kinaandaa mashindano ya aina yake maalum kwa ajili ya watoto wa miaka 16 kwenda chini (Miaka 3 hadi 16) ili kuhamasisha michezo kuanzia umri mdogo.

Mashindano hayo yatafanyika katika Viwanja vya Mnazi Mmoja kuanzia saa 12 asubuhi hadi saa 6 mchana. Zoezi la kwanza mapema siku hiyo itakuwa kugawa T/Shirts (Jezi) za kushiriki zitakazokuwa na alama ya Azania Bank Kids Run kwa washiriki wote watakaokuwa na namba za kushiriki.

Usajili utaanza Alhamisi wiki hii katika matawi yote ya Benki ya Azania jijini Dar es Salaam na ofisi za Chama Cha Riadha uwanja wa Taifa.

Mbio hizo zitakuwa za aina tano; watoto wa kati ya miaka 5 hadi 7 watashiriki kilomita 1, miaka 8 hadi 12 watakimbia kilomita 2 wakati wale wakubwa kati ya miaka 13 hadi 16 watakimbia kilomita 5. 

Wale wadogo wa miaka 2 hadi 3 watashiriki mita 50 na wa miaka 4 watashiriki mita 100 ambazo siyo za ushindani bali burudani baada ya wale wakubwa kumalizika.

Zawadi mbalimbali zitatolewa kwa washindi wa mbio zote kwa kuzingatia jinsia na walemavu nao watapata zawadi zao kwani michezo ni furaha na ni kwa wote. 

Kati ya zawadi zitakazotolewa ni pamoja na fedha taslim ambazo zitaambatana na kufunguliwa akaunti za WATOTO ACCOUNT ya Benki ya Azania.

No comments:

Post a Comment