Kwa Mara ya kwanza Tanzania,mnamo tarehe 5 mwezi wa Sita, Benki ya Azania inakuletea Mbio za Watoto.

Kwa Mara ya kwanza Tanzania,mnamo tarehe 5 mwezi wa Sita, Benki ya Azania inakuletea Mbio za Watoto au unaweza kuziita Kids Run Marathon Hii ni Habari njema kwa Wakazi wa Dar es Salam,hivyo basi Mzazi, Mlezi, unahamasishwa kumleta mtoto wako kuanzia miaka Mitatu mpaka Miaka kumi na Sita waje kushindana na Watoto wenzao Kutakuwa na zawadi kwa kila mtoto na kwa wale washindi watapata zawadi zaidi Jinsi ya kijiandikisha na kushiriki ni rahisi sana fika kwenye tawi lolote la Dar es Salaam lililo karibu na wewe, fomu ni Shilingi 2000/- tu. Watu wote mnakaribishwa.

WADHAMINI wakuu wa Mbio za Watoto za Azania Bank Kids Run 2016, Benki ya

Azania, wametangaza zawadi za washindi wa mbio hizo zitakazofanyika viwanja vya

Mnazi Mmoja, jijini Dar es Salaam, Juni 5.


Akizungumza na waandishi wa habari kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Baraza la

Michezo la Taifa (BMT), Ofisa Masoko Mwandamizi wa Azania Bank, Othman Jibrea,

alisema benki yake inajisikia fahari kuwekeza katika mbio hizo za watoto.


Alizitaja zawadi za mbio za kilomita 5 kuwa ni Sh. 200,000 kwa mshindi wa

kwanza, Sh. 150,000 kwa mshindi wa pili na Sh. 100,000 kwa mshindi wa tatu,

wote wakitarajiwa pia kupata medali, begi lenye vifaa vya shule na vya michezo.


Jibrea alibainisha kuwa mshindi wa kwanza wa mbio za Kilomita 2

atajinyakulia Sh. 100,000, mshindi wa pili Sh. 75,000 na mshindi wa tatu Sh.

50,000, pamoja na medali, begi lenye vifaa vya shule na sare za michezo.


Katika mbio za Kilomita 1, Jibrea alitaja zawadi za washindi kuwa ni Sh.

75,000 kwa mshindi wa kwanza, Sh. 50,000 kwa mshindi wa pili na Sh. 40,000 kwa

mshindi wa tatu, ambao watapata zawadi ya ziada ya medali, begi lenye vifaa vya
shule na michezo.


“Pia washindi wa nne hadi wa 10 wa mbio hizo, watapata kifuta jasho cha Sh.

15,000, begi lenye vifaa vya shule na michezo. Nia ni kuwafanya watoto

watakaoshiriki kutotoka bure mwishoni mwa mashindano, na zawadi zote za fedha
taslimu tutawawekea kwenye akaunti tutakazowafungulia katika Benki ya Azania,”
alisema Jibrea.


Ofisa huyo alifichua kilichowasukuma Azania Bank kudhamini mbio hizo kuwa

ni kurejesha sehemu ya pato lake kwa jamii, lakini pia kuwa sehemu ya

kuiwezesha jamii kujenga kizazi imara kinachoshiriki michezo kwa ustawi wa
taifa.


Kwa upande wake Mratibu wa Azania Bank Kids Run 2016, Wilhelm Gidabuday,

aliishukuru Azania Bank kwa kukubali kusapoti mbio hizo, na kuongeza kwamba kwa

kuwa msingi wa michezo yote ni mbio, basi anaamini Azania imewekeza mahali
sahihi.


“Hakuna mchezo duniani usiohusisha mazoezi ya kukimbia ama usiohitaji

mshiriki kuwa na mbio, iwe soka, ngumi, tenisi, nk. Ndiyo kusema Azania

imefanya uamuzi sahihi na tunawaomba wazazi na walezi wawasajili watoto wao kwa
ada ya Sh. 2,000,” alisema.



Alibainisha kuwa fomu za ushiriki zinapatikana katika matawi ya Azania Bank

popote jijini Dar es Salaam, ofisi za Shirikisho la Riadha Tanzania (RT),

pamoja na Ofisi za BMT zilizoko Samora Avenue katikati ya jiji.

Comments

Popular

GIDABUDAY KUHAMASISHA UJENZI WA KIJIJI CHA MICHEZO TANZANIA LENYE JINA YA MWANARIADHA MKONGWE BW.JOHN STEPHEN AKHWARI

Rio Olympics: Brazil win men's volleyball gold, GB's Joyce takes boxing silver – as it happened

Olympics 2016: Usain Bolt completes sprint double, Jade Jones retains taekwondo title

Rio Olympics: Swimmer Lochte apologises for 'robbery' saga