Latest News

Tuesday, June 14, 2016

Kusitishwa mashindano ya mashule ni kilio kwa maafisa michezo


Baadhi ya washiriki wa mashindano ya UMISETA wakipita kwa mandamano mbele ya mgeni rasmi kwenye uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza Juni 10 2015

Naunga mkono kwa sababu naamini usitishwaji huo ni kupanga upya mpango mkakati wa kuboresha mashindano hayo ili yawe na muendelezo chanya kwa washiriki wenyewe na taifa kwa ujumla.

Maoni yangu binafsi nahisi kwamba mashindano hayo yamekuwa ya kusaka tonge kwa maafisa michezo ambao mimi nawafananisha na wafanyakazi hewa. 

Pia waalimu wanafaidika kwa kula posho kubwa pasipo kujali washiriki wanaendelezwa vipi badala ya kuwapa zawadi na kupiga picha na viongozi kisha kurudi makwao bila kuendelezwa.

Pia kumekuwa na madai kwamba kipindi wapo makambini watoto wa kike hupata matatizo ya (Sexual Harassment) kutoka kwa waalimu na hata wanafunzi wa kiume.

Bilashaka serikali itajipanga upya kuunda system mpya ya uendeshaji wa mashindano hayo ili yasiwe kama mabonanza, bali washindi na wenye talents wakishabainishwa kuwepo na KITUO CHA TAIFA CHA MICHEZO ampapo watapata training ya kujinoa sambamba na kuendeleza masomo yao.

Pia nashauri michezo hiyo itakaporudi upya isiwe chini ya TAMISEMI, bali iwe chini ya wizara ya ELIMU na wizara ya MICHEZO. Ili kila mchezo upate usaidizi wa kitaaluma kutoka kwa Vyama husika vya michezo husika. Mfano; Mpira wa Miguu wasaidiwe na TFF, Riadha wasaidiwe na RT nk.

Pia mashindano hayo ya mashule yawe vigezo vya ajira za vikosi vya Majeshi na Polisi maana huko ni mahala ambapo wataendeleza fani zao.


TUSITAFUTE MBEGU WAKATI SHAMBA HATUNA, MASHINDANO YA MASHULE YASITISHWE HADI KITUO CHA MICHEZO CHA TAIFA KIJENGWE (NATIONAL SPORTS VILLAGE)