Latest News

Wednesday, July 31, 2013

MAADALIZI MABOVU YA WANARIADHA NCHINI YAWAKOSESHA MEDALI KWENYE KILIMANJARO MARATHON 2013

 
 
Gadiel Urio- Wazalendo 25 Blog -Ushirika Moshi
 
 Maandalizi mabovu ya mashindano ya Riadha nchini Tanzania yawakosesha medali wanariadha wakongwe na chipukizi. wakiongea na Wazalendo 25 blog kwa nyakati tofauti wanariadha wakongwe kama vile Fabian Joseph, Phaustin Baha ,Lucian Hombo na Rogath John Stephen Akhwari ,walisema chama cha riadha nchini kimeshindwa kuandaa wanariadha wote katika kiwango cha kimataifa. 
 
'Mshindi wa kwanza katika mashindano ya Kilimanjaro Marathon mwaka 2013 Bw. Lucian hombo ,amesema kuwa uongozi ni mbovu kwa kuwa wanariadha walitakiwa wawekwe kwenye  makambi ili waandaliwe vizuri ,wapate mahitaji mbali mbali kama chakula,maji na vifaa ila haukuwa hivyo. 

pia akaongeza kuwa wanariadha wengi wanaojitahidi kushinda ni wale walioandaliwa na Jeshi la kujenga Taifa na jeshi la magereza. akaongeza kuwa waandaaji wa kilimanjaro marathon walitangaza kuwa kuna pesa zilitolewa ili kusaidia maandalizi ya riadha ila hazikuonekana na hakuna kambi yeyote iliowekwa popote' alihoji Bw. Lucian Hombo.
 
'Waandaji wa kilimanjaro marathon hawana viwango vya kimataifa ,kwa kuwa mara nyingi katika kuanza kwa mbio nyingi za kimataifa ,wale wanariadha wakongwe huwekwa mbele na kufuatiwa na wale wengine chipukizi ila hapa haukufanyika hivyo, hiyo ilipelekea mshiriki wa kimataifa wa mbio za nusu marathon duniani Bw. Phaustin Baha na mwenzake Fabian Joseph Kushindwa kufikia lengo lao la ushindi 'alisema mwanariadha wa kimataifa Bw. Rogath Stephen.
 
'Waandaaji na viongozi wa michezo ya kimataifa wanatakiwa wapewe semina ya jinsi ya kuandaa mshindano hayo na wapewe elimu kuhusu kutofautisha wanariadha wa kimataifa na wanariadha chipukizi ,kwa kuwa mkimbiaji wa kimataifa ana hitaji huduma ya kipekee ili asiumizwe na rundo la watu wanaokimbia kwa mara ya kwanza ,hiyo itamsaidia yeye kuendelea kushiriki mashindano mengine ' alisema Bw. Phaustin Baha.
 
Kwa upande wa jirani zetu wakenya walipata medali nyingi katika mbio hizo:
 

  Kama vile Kipsang Kipkemoi alishinda mbio za kilometa 42 akifuatiwa na Nafasi ya pili hadi ya tano kwa wanaume ni Julius Kilimo, Dominick Kiagor, Onesmo Maithiya Loshile Moikarikunyakua nafasi ya kwanza  katika mbio hizo za mwaka huu upande wa wanaume na Wanawake ilinyakuliwa na Mwana dada Edna Joseph alebeba Medali ya Dhahabu na medali zingine zilikwenda kwa Eunice Muchiri, Frida Too, Rosaline David na Jane Kenyara. 
Mwana dada Sarah Ramadhan Makera alinyakua medali ya dhahabu kwa kuibuka mshindi wa kwanza mbele ya mkenya Vicomi Chepkemoi huku nafasi ya tatu ikichukuliwa na mtanzania mwingine Failuna Makanga.

Nafasi ya nne ilienda kwa Joyce Kiplimo wa Kenya aliyefuatiwa na mwenzake Pauline Muchiri  kasha Mtanzania Catherine Tuku alishika nafasi ya sita na zilizosalia hadi nafasi ya kumi zikienda kwa Nchi ya Kenya ambao ni Nancy Kotch, Jacinta Mboani, Florence Cheruiyot na Phylas Jelagat. 

Wakimbiaji wa Kenya wakipongezana baada ya kufanya vizuri katika mbio hizo.

Eunice Muchiri akimalizia mbio za Kilometa 42 Wanawake, katika Mbio za Kilimanjaro Marathon 2013.

Kocha Mkuu wa timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ Kim Poulsen akimaliza kukimbia Kilometa 21 katika mbio za nyika za Kilimanjaro 2013. Poulsen amedhihirisha kuwa ni mwanamichezo na kuwa kocha wa Kwanza wa Timu ya Taifa kushiriki mbio hizo tangu kuanzishwa kwake miaka 10 iliyopita.
Mbio hizi wapo waliokuwa wanazungukwa kama hapa wanavyopishana njiani. Kulia wakienda huku Kushoto wakirudi kumaliza.
 Kocha Mkuu wa Timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ Kim Poulsen akikimbia mbio hizo za kilometa 21.  
Mkongwe wa Mbio za nyika akikimbia Kilometa 21. Babu huyu alimaliza mbio hizo. Picha na Father Kidevu Blog

No comments:

Post a Comment