GIDABUDAY AZUNGUMZA NA VYOMBO VYA HABARI JIJINI ARUSHA


Wadau wa Michezo nchini wakizungumza na vyombo vya habari jijini Arusha;kutoka kushoto ni Gadiel Urio PR wa Shughuli hiyo, Rogath John Stephen(Mwanariadha wa kimataifa na Mtoto wa John Stephen Akhwari) , Bw. Wilhelm Gidabuday ambae ni mwanariadha na mwanaharakati wa Michezo Tanzania na Phaustin Baha Sule Mwana Riadha na Mshindi wa medali ya nusu marathon.
Kutoka kushoto ni Rogath John Stephen ,mwanariadha wa kimataifa na mtoto wa mwanariadha maarufu duniani Bw. John Stephen Akhwari ,Phaustin Baha Sulle mshindi wa medali ya fedha katika nusu marathon na Mwanaharakati wa michezo Tanzania Bw. Wilhelm Gidabuday.
Hapa wakipewa maelekezo na PR wa shughuli hiyo,kabla ya kuanza kwa mazungumzo na Vyombo vya Habari ,katika mkutano wa vyombo vya habari vilivyofanyika Jijini Arusha.  .


**********************
  Na Gadiel Urio -Arusha

“Sisi  kama wadau wakubwa na wazalendo wa michezo Tanzania ,tumeamua kuanzisha tukio hili la harambee,                   kupitia kukimbia mbio za kupokezana vijiti (RELAY MARATHON) , ili kuchangisha pesa ya kuanzisha  kiijiji cha kitaifa cha Michezo nchini Tanzania .pia  kijiji hicho cha michezo Tanzania  kitaitwa “John Stephen Akhwari National Sports Village” ,kwa heshima ya mwanariadha huyo wa kimataifa alieiletea sifa nchi ya Tanzania kwa kukimbia bila kukata tamaa ,hata aliposhindwa alidiriki kusema “Nchi yangu haijanituma kuja kuanza mashindano: bali kumaliza Mashinadano. Pia  baada ya kuona michezo mingi Tanzania imekosa vituo vyenye hadhi ya kimataifa vya kufanyia mazoezi yenye ubora wa kimataifa,ili kupata medali ndani na nje nchi yetu. Hivyo  tukakaa na baadhi ya wanariadha wazalendo nchini kama vile,Phaustin Baha na Rogart John Stephen ,ili tufanye tukio hili la kihistoria ambalo hakuna mwingine aliewahi kujaribu kulifanya “alisema Wilhem Gidabuday
“Mashindano hayo yatakuwa ya  mbio za kupokezana vijiti yaani (RELAY MARATHON) kuanzia Magogoni jijini Dar es Salaam (IKULU) na kumalizia jijini  Arusha (Sheikh Amri Abeid) kupitia barabara kuu itokayo Dar es Salam hadi Arusha, yenye takribani kilomita zisizopungua mia saba (700 Km). Mbio hizo  zitahusisha wanariadha  wa tano maarufu na  wazalendo na ambao wamewahi kukimbia na kuiletea nchi yetu sifa kimataifa”.aliongeza Bw. Gidabuday
Malengo ya Mbio hizi ni:
Moja ; kuwezesha kuanzisha kijiji cha michezo Tanzania kulingana na jeografia ya nchi yetu ilivyo, kuwa na maeneo ya nyanda za juu kaskazini na kusini ambamo hali ya hewa inaruhusu michezo mingi kufanyika ikiwemo mchezo wa riadha. hili litasaidia kupata wanamichezo wazuri na wenye lengo la kuiletea sifa na medali nchi yetu kitaifa na kimataifa na kuongeza ajira kwa wanamichezo wetu.
Pili ;kwa kuwa Raisi wetu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Dr. Jakaya Kikwete ni msikivu ,anapenda michezo na alitambua mchango mkubwa wa mwanariadha mkongwe Bw. John Stephen Akhwari na kumpa Tuzo ya miaka 51 ya Uhuru wa Tanzania ,ndipo tukapendekeza kijiji hiki cha michezo kiitwe John Stephen Akhwari, ila kijiji hiki ni mali ya serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Mashindano haya yanatarajiwa kufanyika kabla ya mwezi wa sita  mara tu tutakapowapat a wahisani,Serikali na wadau wengine wa michezo kujitokeza na  kuwezesha jambo hili kutimia . hivyo tunaiomba serikali ,wadau mbalimbali wa michezo nchini pamoja na wahisani wajitokeze ili kutimiza lengo hili la kitaifa la kuanzisha kijini cha michezo cha John Stephen Akhwari.
Mwisho ;Mwaka ujao wa 2014 tunatarajia kukimbia mbio zingine kutoka Bagamoyo hadi ujiji ,katika miaka 50 ya mapinduzi ya Zanzibar ,lengo ni kuhamasisha na kuchangisha pesa za ujenzi wa kituo hicho cha kimataifa. 

Comments

Popular

GIDABUDAY KUHAMASISHA UJENZI WA KIJIJI CHA MICHEZO TANZANIA LENYE JINA YA MWANARIADHA MKONGWE BW.JOHN STEPHEN AKHWARI

Rio Olympics: Brazil win men's volleyball gold, GB's Joyce takes boxing silver – as it happened

Olympics 2016: Usain Bolt completes sprint double, Jade Jones retains taekwondo title

Rio Olympics: Swimmer Lochte apologises for 'robbery' saga