Posts

Showing posts from June 29, 2014

HAFAI TENA: Cheka mbaroni, ampiga mtu baa Morogoro

Image
BONDIA FRANCIS CHEKA JESHI la Polisi mkoani hapa linamshikilia bingwa wa ngumi za kulipwa duniani, Francis Cheka ‘SMG’ kwa tuhuma za kumchapa Meneja wa baa ya Vijana Social Hall iliyopo Kata ya Sabasaba, Manispaa ya Morogoro.  Kwa mujibu wa maelezo ya meneja huyo, Bahati Kabanda ‘Masika’ (39), Cheka alifika katika baa hiyo majira ya jioni na kuanza kumtukana na kumshambulia kwa maneno machafu kisha kumvamia na kuanza kumchapa ngumi na mateke sehemu za tumboni. Kwamba ni tukio la Juni 2, mwaka huu katika baa hiyo inayomilikiwa na promota wa ngumi za kulipwa mkoani hapa, Zumo Makame. Kabanda amedai wakati akipewa kichapo na Cheka, hakuna mtu aliyesogea kuamulia ugomvi huo kutokana na watu kumuogopa bondia huyo aliyewahi kuwapiga mabondia wa ndani na nje ya nchi. Alidai Cheka alifika katika baa hiyo na dalili za kulewa pombe na baada ya kuondoka, wasamaria wema walimchukua yeye hadi katika hospitali ya rufaa ambako alilazwa na kupatiwa vipimo na matibabu ya maumivu aliyoy...

SHABANI HIKI: Ninaimani timu ya riadha itailetea heshima Tanzania

Image
Timu ya wanariadha waliokuwa Ethiopia kwa mazoezi ya maandalizi ya mashindano ya Jumuia za Madola imerejea nchini jana. Katikati ni kocha aliyefuatana na timu Ndg. Shabani Hiki. Wanariadha hao waliowasili nchini kupitia uwanja wa ndege wa Mwalimu Julius Nyerere waliahidi kuiletea heshima Tanzania kwa kuzoa medali katika mashindano yatakayofanyika Glasgow Scotland mwishoni mwa mwezi huu wa July. Mwanzoni mwa mwezi June mwaka huu serikali ilitoa fedha za makambi kupitia wizara ya Mambo ya Nje katika harakati za kuinusuru Tanzania kupata medali katika mashindano hayo ya Commonwealth Games yajulikanayo pia kama "Family Games" zinazoshirikisha nchi zote zilizowahi kuwa chini ya himaya ya Uingereza.