Ruksa serikali kushiriki kukimbiza kifimbo cha Malkia lakini haramu serikali kuhoji ufisadi ndani ya TOC
Rais Kikwete akiwa na timu ya Olimpiki London 2012 Je serikali ya Tanzania ni serikali ya kuchezewa kihivyo na genge la mafisadi wanaijidai wao hawaguswi na serikali? Je raisi wetu Mheshimiwa Jakaya Kikwete atafurahia ‘kijifimbo’ cha Malkia badala ya kupewa ripoti ya USD 100,000 zilizopakuliwa India? Kama kawaida ya sera yetu ya “UTAIFA KWANZA” tunaiomba serikali kupitia Baraza la Michezo Tanzania (BMT) na Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo watafakari mambo yafuatayo: - Kwamba TOC inauma na kupuliza; wanatabasamu kwa serikali wakati wanajiseti kwa “ P icture Perfect” pale tu wanapotaka kudanganya ulimwengu kwamba wao ni vinara nchini. - Kwamba TOC ipo radhi kumpata rais wa Jamhuri ya Muungano ajumuike nao ili wazitumie zile picha kuchota fedha ambazo wanajengea mahekalu yao watanzania tukiishia patupu. - ...