Posts

Showing posts from November 2, 2014

BUTIAMA: Ziara yangu nyumbani kwa baba wa taifa

Image
Safari yangu ya kuingia ndani ya boma la baba wa taifa ilianzia hapo mlangoni ambapo hisia za kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere zilinijia ghafla.   Hili jumba ndilo linalohifadhi kaburi la baba wa taifa, kimsingi ufikapo hapo utapata kujua historia kamili ya jinsi uhuru wetu ulivyopatikana. Utajifunza mengi kwa kuona mwenyewe na pia utapata kuelezwa usiyoyafahamu.   Sanamu ya baba wa taifa! Bilashaka watanzania tutajitahidi kumuenzi baba wa taifa kwa vitendo.