ARCHIVE STORY: Dabusi Fc yatwaa ubingwa Gidabuday Cup
Manyara: Timu ya Dabusi imetwaa ubingwa wa mashindano ya Gidabuday Cup kwa kuichapa Nangwa kwa mabao 3-2 katika fainali iliyochezwa kwenye Uwanja wa Nangwa VTC Wilayani Hanang’. Katika mchezo huo mabao ya Dabusi yakifungwa na Yasini Zuberi kwa mkwaju wa penalti, huku bao la pili alijifunga beki wa Nangwa, Jackson Jolwa kabla ya Deograsia John kumalizia bao la tatu. Wakati mabao ya Nangwa yalifungwa na Nathan Matembo kwa mkwaju wa penalti na Gift Oscar. Michuano hiyo iliyoanza Septemba tatu kwa kushirikisha timu tisa ilikuwa na lengo la kumpongeza katibu mkuu wa RT, Wilhelm Gidabuday kwa juhudi anazozifanya kwenye michezo hapa nchini. Mgeni rasmi katika mchezo huyo alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Hanang, Sara Ally aliwasihi vijana kupenda michezo kwa kuwa ni ajira nzuri. “Asilimia kubwa ya pato la nchi kwenye mataifa yaliyoendelea yanachangiwa na wanamichezo na hata ukifuatilia watu wenye vipato vizuri katika ulimwengu wa sasa ni wanamichezo hivyo hupashwi kukata tamaa kama umeweka ma