KAULI YA NYAMBUI NI KIPIMO TOSHA CHA UDHAIFU WA UZALENDO WETU
Suleiman Nyambui / Mtanzania asiyejali sheria wala uzalendo KATI ya vipindi vya michezo redioni ambavyo hunipita kwa nadra sana ni kile cha Radio One Stereo. Siku chache zilizopita, nilikuwa nikifuatilia namna Maulid Kitenge alivyokuwa akimhoji Katibu Mkuu wa Chama cha Riadha Tanzania (RT), Selemani Mujaya Nyambui. Kitenge alikuwa akitaka kujua sababu ya timu ya Tanzania iliyoshiriki michuano ya Jumuiya ya Madola kurejea nyumbani bila ya hata kipande cha medali. Nyambui ambaye katika sauti yake unaweza kubaini mengi, alizungumza mambo ya ajabu ambayo hauwezi kutarajia kiongozi au mwanamichezo mwenye sifa yake anaweza kuzungumzia. Mwanariadha huyo wa zamani ambaye unaweza kumwita ni kati ya mashujaa waliowahi kuchukua medali na kuileta nyumbani kupitia michuano ya Olimpiki, alikuwa akizungumza sawa na mtu aliyekuwa hayuko vizuri, labda kwa uchovu au ni yule asiyejali tu. Wakati Kitenge akieleza alitaka kujua kwa nini timu hiyo haikuleta medali, Nyambui hakufafanua lo