Posts

Showing posts from May 6, 2018

Nyota Kibao Washiriki Ngorongoro Race 2018

Image
Mbio za Ngorongoro Race kabla ya kuanza mwaka jana. Na Mwandishi Wetu WANARIADHA nyota wamethibitisha kushiriki mbio za mwaka huu za Ngorongoro Race zitakazofanyika Aprili 21, imeelezwa. Mkurugenzi wa mbio hizo, ambazo zinafanyika kwa mwaka wa 11 sasa, Meta Petro alisema jana kwa njia ya simu kuwa, tayari wanariadha wengi nyota wamethibitisha kushiriki mbio hizo. Wanariadha wakichuana katika mbio za mwaka jana mjini Karatu. Baadhi ya wanariadha nyota waliothibitisha kushiriki ni pamoja na Fabian Joseph, Said Makula, Fabian mdogo, Dickson Marwa, Sarah Ramadhani, Jaquline Sakilu, Stephano Huche, Failuna Abdi na wengine. Makula, Sarah na Huche wamo katika timu ya Tanzania iinayoshiriki Michezo ya 21 ya Jumuiya ya Madola iliyoanza Gold Coast, Australia kuanzia Aprili 4 hadi 15. Ofisi ya Ngorongoro Race iliyopo Karatu mkoani Arusha. Petro alisema kuwa tayari zaidi ya wanariadha 200 wamejiandikisha kutaka kushiriki mbio hizo, ambazo zimekuwa zikifanyika katika kipindi cha