Posts

Showing posts from January 12, 2014

Kikwete awatia hofu watarajiwa wa uwaziri huku wengine wakifunga novena kumomba mungu wasipigwe chini

Image
James Lembeli "The Man Ikulu yageuka mbingu ya pili kwa kile kinachodaiwa sala zote lazima iombe huruma za mungu angalau rais awateue. Hadi hii leo hii ni takriban mwezi mzima umepita tangu kutenguliwa kwa mawaziri wanne baada ya kuguswa moja kwa moja na kashfa ya Operation Tokomeza Ujangili. Mawaziri waliolazimika kujiuzulu ni pamoja na Emmanuel Nchimbi - Mambo ya ndani, Shamsi Vuai Nahodha - Ulinzi, David Mathayo – Mifugo na Khamis Kagasheki – Maliasili na Utalii.  Pigo lingine kwa baraza la mawaziri ni pale Tanzania ilipompoteza aliyekuwa waziri wa fedha Dr. William Mgimwa aliyefariki dunia masaa machache kabla ya mwaka 2014 kuanza. “Rais Kikwete kipindi hiki ana kazi nzito ya kufanya; siyo kuteua mawaziri pekee! Kumbuka wabunge wa bunge maalum la katiba nao wapo katika process ya kuteuliwa” Chanzo cha kuaminika kilisema. “Anaweza kuamua kuendelea na uteuzi wa wabunge wa katiba ndipo atangaze zote kwa pamoja” mtoa habari alisema hayo kwa kifupi.  A

OFISI ZA BUNGENI: MHE. MIZENGO PINDA AKAGUA MAENDELEO YA UKARABATI WA JENGO LA BUNGE LA TANZANIA

Image
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiwa ameketi wakati akikagua marekebisho yanayofanyika katika ukumbi wa Bunge mjini Dodoma Januari 18, 2013 ikiwa ni maandalizi ya Bunge la Katiba linalotarajiwa kuanza mwezi ujao. Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu. (Picha ya Juu) Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akikagua kazi ya uwekaji viti vipya katika ukumbi wa Bunge mjini Dodoma Januari 18,2014 ikiwa ni maandalizi ya Bunge la Katiba linalotarajiwa kuanza mwezi ujao. (Picha ya Chini)

Wabunge watapeliwa: Wamwaga fedha kusaka uwaziri, Ikulu yatoa kauli nzito kuwaonya, JK kutangaza Mawaziri wapya leo

Image
IKULU imewaonya wabunge wenye uchu wa kuwa mawaziri na mawaziri wanaotaka kubaki kwenye madaraka hayo wasikubali kurubuniwa na matapeli wanaojifanya maofisa Usalama wa Taifa ambao wanawataka kutoa fedha ili wasaidiwe kupata uwaziri. Onyo hilo limetolewa wakati Rais Jakaya Kikwete akitarajiwa kutangaza Baraza jipya la Mawaziri leo baada ya kuwang’oa mawaziri wanne na mmoja kufariki dunia. Akizungumza na Tanzania Daima jana, Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue alisema hakuna sababu za wabunge kukubali kutapeliwa kwa ajili ya kusaka uwaziri kwani mwenye mamlaka ya uteuzi ni Rais Kikwete na hakuna mwenye uwezo wa kuingilia uteuzi wake au kumshawishi afanye upendeleo. Mbali ya kuwaonya wabunge na mawaziri hao, Balozi Sefue pia aliwaonya matapeli wanaotumia jina la Ofisi  ya Rais Ikulu kujifanya maofisa wa Idara ya Usalama kuwarubuni watoe fedha ili wawasaidie kuingia kwenye Baraza jipya la Mawaziri. Kwa mujibu wa Balozi Sefue, wabunge wanapaswa kuwapuuza matapeli

Baraza la mawaziri joto nyuzi 100: Taarifa zinasema rais Kikwete jana alikutana na makamu wake Dr. Gharib Bilal Ikulu

Image
Mh. Rais Dr.Jakaya Kikwete Wakati Watanzania wakisubiri kwa hamu mabadiliko ya Baraza la Mawaziri, Rais Jakaya Kikwete amekuwa akikuna kichwa kupanga safu yake huku Ikulu ikiwataka wananchi kuwa watulivu katika kipindi hiki. Tangu mawaziri wanne, Dk Emmanuel Nchimbi (Mambo ya Ndani), Shamsi Vuai Nahodha (Ulinzi na JKT), Balozi Khamis Kagasheki (Maliasili na Utalii) na Dk David Mathayo (Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi) walipovuliwa nyadhifa zao ikiwa ni hatua ya kuwajibika kutokana na madhila yaliyowapata wananchi kutokana na Operesheni Tokomeza Ujangili, na kifo cha aliyekuwa Waziri wa Fedha, Dk William Mgimwa, kumekuwa kuna kila aina ya uvumi. Hata hivyo, kitendawili kilichobakia ni siku gani hasa Rais Kikwete atakapotangaza mawaziri wapya kwani hata wasaidizi wake wamekuwa wakikwepa kuzungumzia suala hilo na kuwataka wananchi kuvuta subira.   Taarifa zilizofikia gazeti hili jana, zilieleza kuwa Rais Kikwete alikutana na Makamu wa Rais, Dk Mohamed Gharib Bilal Ikulu kuj