Nyambui: Tujitoe Madola
KATIBU Mkuu wa Shirikisho la Riadha Tanzania (RT), Suleiman Nyambui, ameitaka Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC), kuifuta Tanzania kushiriki mashindano ya kimataifa hadi itakapokuwa imefanya maandalizi ya kutosha. Kauli hiyo ya Nyambui imekuja wakati akitoa maoni yake juu ya ushiriki wa Tanzania katika mashindano ya Jumuiya ya Madola yatakayofanyika Glasgow, Scotland baadae mwaka huu. Akizungumza na Tanzania Daima jijini Dar es Salaam jana, Nyambui alisema kama nchi inataka kupata mafanikio katika mashindano hayo inapaswa kujipanga kuanzia ngazi ya vijana kwani ndiyo msingi wa mafanikio ya michezo yote. Alisema kinachoiponza Tanzania ni maandalizi. “Mbona zamani walifanya vizuri kwa nini sasa hivi washindwe,” alisena na kuongeza kwamba Tanzania ya sasa si kama ile ya zamani wakati wao wanaiwakilisha nchi katika mashindano mbalimbali. “Siku zote shule ndiyo zinaibua vipaji, kama zikiwa nzuri hata timu za taifa zitakuwa nzuri pia,” alisema Nyambui ambaye pia ni mjumbe ...