Posts

Showing posts from February 23, 2014

Jamali Malinzi, wadau kumlipa Kim

Image
Jamali Malinzi Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi jana alitangaza rasmi kuondolewa kwa kocha Kim Poulsen, lakini akashindwa kueleza sababu za kuachana na mwalimu huyo kutoka Denmark. Malinzi, ambaye uongozi wake ulifanya kituo cha kuteua wachezaji wa timu ya taifa badala ya kazi hiyo kufanywa na kocha, pia jana aliongeza alitangaza kuwa fidia ya kuvunjwa kwa mkataba wa Poulsen zitalipwa kwa ushirikiano baina ya TFF na wadao, ambao pia hakuwataja. Poulsen, ambaye analipwa mshahara na serikali kutokana na ahadi ya Rais Jakaya Kikwete, ana mkataba unaoisha Mei mwakani  na alipewa kazi hiyo baada ya kuonyesha mafanikio kwenye timu za vijana. Hivyo, kuvunjwa kwa mkataba huo kutalifanya Shirikisho hilo limlipe Poulsen mishahara yake ya miezi sita kulingana na mkataba wake. “Jukumu la kulipa gharama za kuvunja mkataba zitabebwa na TFF na baadhi ya wadau wa soka watatusaidia nusu ghar

Oscars 2014: When Will Leonardo DiCaprio Finally Win?

Image
Leonardo DiCaprio After a stellar award season, the 86th Academy Awards are this weekend and —  by almost anyone’s measure  — Matthew McConaughey has a lock on the Best Actor Award. Though this year has seen fierce competition from his co-nominees Chiwetel Ejiofor, Christian Bale, Bruce Dern and  Leonardo DiCaprio  (more on him in a minute), there’s been an undeniable groundswell of support for McConaughey.  His role in  Dallas Buyers Club  certainly checks all the boxes typical of an award-winning performance: he lost a dramatic amount of weight for the role; he plays a real-life character who not only suffers from a deadly illness, but also heroically fights a weighty cause for others; and he’s already proven at other award ceremonies that he can hit a humble, charming and funny acceptance speech out of the park. Few would be surprised to see him snag the statue come Sunday night. However, it’s often the case that Academy doesn’t necessarily reward individual performances,

Sports Diplomacy: Waziri Membe kupeleka wanariadha 40 nje ya nchi

Image
Mhe. Bernard Membe Tanzania inaelekea kupata nafasi ya kupeleka timu ya riadha nchini China, Ethiopia na Uturuki kwa maandalizi ya kuwanoa vijana kwa mashindano ya madola na kwa msaada wa waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Bernard Membe. RT imeonyesha dalili za kuchagua wanariadha mezani badala ya mashindano ya wazi ili kufanya mchujo wa kidemokrasia.  Mfumo ambao nchi za wenzetu kama Kenya wanafanya ili kuepusha upendeleo wa aina yoyote. Katibu wa RT Sulemain Nyambui amekaririwa na vyombo vya habari akidai kupeleka majina kwa waziri Membe. 'Wazalendo na wapenda haki tunadhani ipo haja ya kuandaliwa mashindano maalum yatakayopewa viwango kadha ambayo wakimbiaji wakifikia ndio wachaguliwe kwa uwazi badala ya kumpa mwanya kiongozi  moja kumpendelea ndugu ama jamaa yake' Kuna tetesi kwamba kuna vijana na makocha ambao wamehakikishiwa safari hizo kwa ahadi maalum kwamba wakijiandaa kutoa chochote watahakikishiwa wanasafiri bila kujali uwezo

Tanzania Tennis Association kuadhimisha Siku ya tenisi duniani

Image
M/ Kiti wa TTA Methusela Mbajo / katikati Jumamosi wiki hii ( March 1 st ) chama cha tenisi Tanzania (TTA) kitaungana na vyama vya tenisi duniani pamoja na wadau kusherehekea siku ya tenisi ulimwenguni. Maadhimisho hayo yatafanyika katika viwanja vya Dar Es Salaam Gymkhana Club ambapo maadhimisho yataambatana na mafunzo ya bure kwa watoto na wakubwa watakaopenda kujifunza mchezo wa tenisi. Shughuli zitaanza saa tatu asubuhi hadi saa nane mchana, mafunzo yataendeshwa na makocha waliobobea wa tenisi wakiwemo   Kiango Kipingu na Hassan Kassim . Watanzania mnakaribishwa kiingilio ni bure, ‘njoo uangalie, njoo ujifunze, njoo ufurahi’

KENYAN DOUBLE FOR KAROKI AND WACERA AT WORLD’S BEST 10K

Image
24 FEB 2014   REPORT   SAN JUAN, PUERTO RICO Kenyans Bedan Karoki and Mary Wacera made a brilliant debut on the Teodoro Moscoso bridge and prevailed over a large African contingent to become the 2014 champions at the World’s Best 10K, an   IAAF Gold Label Road Race , whose 17th edition was held Sunday (23) afternoon in the Puerto Rican capital of San Juan. For world and Olympic 10,000m finalist Karoki and 2006 world junior bronze medallist Wacera, it was their most important road win of their international career. How the races unfolded With temperatures hovering around 27°C, a large group of about 20 runners, led by New Zealander Zane Robertson, followed a pedestrian pace, covering the first three kilometres in nine minutes. The lead pack hit the half-way mark in 14:26 and was reduced to six men after eight kilometres. Karoki made his move with two kilometres to go, gaining a 50-meter lead that increased by the time he crossed the finish line in 28:35, the second-slow

KATIBA: Nyongeza ya posho yagonga mwamba

Image
Bunge la Katiba Madai ya Wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba kutaka nyongeza ya posho ya vikao vya Bunge hilo yamegonga mwamba, Mwananchi limebaini.  Habari kutoka ndani ya kamati iliyoundwa na Mwenyekiti wa Muda wa Bunge la Katiba, Pandu Ameir Kificho ili kufuatilia madai hayo, zimedai kuwa baada ya uchunguzi wa kina, wajumbe wa kamati hiyo hawakuona sababu ya kupendekeza posho hizo kupandishwa. Taarifa hizo zilidai kuwa wajumbe hao wamefikia uamuzi huo baada ya kupitia viwango vya posho vinavyolipwa na  Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Serikali na Mashirika ya Umma. Pia kamati hiyo ilichambua viwango vya posho walivyolipwa wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba na viwango vya posho ya kujikimu vya Sh80, 000 kwa siku wanavyolipwa watumishi wa Serikali.  “Hili jambo linahitaji busara sana na kutazama mazingira ya nchi pia, kwa hiyo wajumbe wale baada ya kuoanisha viwango vya posho vya taasisi mbalimbali wameona Sh300,000 zinatosha,” alisema mmoja wa wajumbe ambaye

Waziri Mukangara mgeni rasmi Kilimanjaro Marathon

Image
Dr. Fenella Mukangara - Waziri Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo, Mhe. Dk. Fenella Mukangara anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye mbio mbio za 12 za Kilimanjaro Marathon ambazo zinatarajiwa kufanyika Jumapili ijayo tarehe 2 Machi, 2014 mjini Moshi. Aggrey Marealle, Mkurugenzi Mkuu wa Executive Solutions, waratibu wa mbio hizo alisema jana kwamba Dr. Mukangara amekubali kuwa mgeni rasmi na atahuduria sherehe ya utoaji zawadi ambapo atatoa zawadi kwa washindi kumi wa mbio defu za kilomita 42 maarufu kama Full Marathon kwa wanaume na wanawake.  “Uwepo wa waziri ni ishara ya uungaji mkono tukio hili na ameeleza kufurahishwa kwake na maandalizi ya hali ya juu ya Kilimanjaro Marathon. Dk. Mukangara ameeleza mara kadhaa kwamba serikali inaunga mkono Kilimanjaro Marathon kwa kutambua mchango wake michezo, utalii na uchumi,” alisema Marealle. Marealle aliongeza kwamba baada ya sherehe ya utoaji zawadi Waziri ataungana na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro na mpenda michezo Mhe.