Posts

Showing posts from May 11, 2014

Good coaching equals winning athletes, exceptional people

Image
“Good coaching, like good leadership, is having the ability to cause positive change,” says Dr. Kent Schlichtemeier, Concordia Hall of Fame Women’s Basketball coach and professor of Principles of Coaching and Leadership at Concordia University Irvine. In coaching, he says, “you’re striving to cause positive change in the lives of athletes while helping them compete successfully.” In addition to creating winning athletes on the field, good coaching is about creating championship people through character development, says Dr. Schlichtemeier. “Character comes from the Greek meaning ‘to engrave.’ So parents, teachers and coaches, and clergy seek to engrave positive values onto the hearts of children from the day they’re born,” he says. “Good coaches strive to reinforce the parent’s pursuit of inculcating positive values into the lives of kids so that they will be successful, productive, happy citizens throughout their lives.” Because coaches have an athlete’s undivided atte

Wambura hatishiki pingamizi Simba

Image
Mgombea urais wa klabu ya Simba, Michael Wambura, amesema hana hofu na watu wanaomtishia kumuwekea pingamizi ili asigombee nafasi hiyo kwenye uchaguzi utakaofanyika Juni 29 jijini Dar es Salaam. Baadhi ya wanachama wa klabu hiyo walidai klabuni hapo mwishoni mwa wiki kuwa watamuwekea pingamizi mgombea huyo kwa madai kuwa hana vigezo vya kuwania nafasi hiyo. Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Wambura alisema hawezi kurudi nyuma katika dhamira yake ya kuwania uongozi Simba na kwamba wanaotaka kumpinga wafanye hivyo. Alisema kuwa anawania uongozi kwa kuwa ana vigezo na sifa za kuwania hivyo wanaotaka kumpinga waandae hoja zao. "Siwezi kusikiliza maneno ya watu... hao wanaotaka kunipinga wafanye hivyo lakini dhamira yangu ni kuwania uongozi ndani ya Simba ili nitoe mchango wangu na kuindeleza Simba," alisema Wambura ambaye amewahi kuenguliwa kugombea uongozi hatua tatu. Wambura alienguliwa kwenye uchaguzi uliopita wa Simba kwa kosa la kufungua kesi m

Taswa kuandaa mjadala Jumuiya ya Madola

Image
CHAMA cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (Taswa), kimeanzisha utaratibu wa kuandaa midahalo mbalimbali ya masuala ya michezo kila Jumatano ya kwanza ya mwezi, ambapo kwa kuanzia wataanza na uwakilishi wa Tanzania katika michezo ya Jumuiya ya Madola.   Kwa mujibu wa Katibu Mkuu wa Taswa, Amir Mhando, watakuwa wakialika wataalamu kutoka vyama vya michezo, wanamichezo maarufu, wahariri wa habari za michezo na waandishi wa habari za michezo, ambao watakuwa wakijadili hoja husika. Alisema huo ni uamuzi wa Kamati ya Utendaji iliyokutana Jumatatu, ambapo mambo mbalimbali yalijadiliwa, na kuongeza kuwa kutakuwa na wazungumzaji maalumu kuhusu mada husika, ambapo wageni waalikwa watachangia kwa nia ya kuboresha kwa maslahi ya ustawi wa michezo hapa nchini. Mhando alisema kwa kuanzia mjadala huo utafanyika Juni 4 katika ukumbi ambao utatangazwa hivi karibuni, na mada itakuwa nafasi ya Tanzania katika Michezo ya Jumuiya ya Madola itakayofanyika Glasgow, Scotland kuanzia Julai 23 h

2016 RIO DREAMS: I am back running again after a long holiday break

Image
Yes I know this will be hard for people to believe! WHAT if I make it to Rio representing Tanzania! And WHAT if my son makes it to RIO representing United States of America in one single Olympic Games? Will it be a history or what? Hahaha I don’t know but ‘HELL YES’ Anything can happen!

HATARI: Malinzi mfukuze Nyambui RT

Image
Ni Jumatatu nyingine tena tunakutana wadau wa Uwanja wa Kuchonga, kama kawaida tukipeana changamoto za kispoti ili kuchochea ufanisi katika sekta hii muhimu katika jamii. Bila shaka mu wazima wa afya na mnaendelea na majukumu ya ujenzi wa taifa kama kawaida, ila kwa wale ambao hali zao si shwari kwa namna moja ama nyingine, tunawaombea nafuu ya mapema. Kama ada, kwa manufaa ya wale ambao hatukuwa nao wiki iliyopita, tupeane dondoo japo kwa ufupi kile kilichojiri Jumatatu iliyopita. Wiki iliyopita tuliangalia sakata la usajili wa aliyekuwa kiungo wa Yanga, Frank Domayo, ambaye alinyakuliwa na mabingwa wa soka Tanzania Bara, Azam FC, tukio lililowagusa mashabiki na wadau wengi wa soka hapa nchini. Lakini tulichokizungumzia, si kusajiliwa kwake Azam, bali jinsi Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), lilivyojiingiza katika suala hilo kwa mgongo wa tukio hilo kufanyika kambi ya timu ya taifa, Taifa Stars, kisha kuamua kumteua Wakili Wilson Ogunde, kwa kile kilichoitwa kuc

Tupa: Sililii safari, bali jina langu kutumika

Image
Mwl. Samwel Tupa akitoa hoja KOCHA maarufu wa riadha nchini, Samwel Tupa kutoka Arusha, amefafanua kwamba anacholilalamikia Shirikisho la Riadha Tanzania (RT), ni jinsi jina lake lilivyotumika kama kocha aliyeondoka na wachezaji waliokwenda New Zealand kuweka kambi kwa ajili ya maandalizi ya mashindano ya Jumuiya ya Madola yanayotarajiwa kufanyika Julai mwaka huu, Glasgow Scotland. Jina la kocha huyo lilitangazwa katika vyombo vya habari, kwamba ameondoka na wanariadha hao, lakini badala yake alikwenda Katibu Mkuu wa RT, Suleiman Nyambui, kama kocha wa wanariadha na yeye kuachwa bila taarifa. Akizungumza na Tanzania Daima kwa njia ya simu akiwa jijini Arusha, Tupa alisema anacholalamika yeye ni kwanini uongozi wa RT uliamua kutumia jina lake hadi dakika za mwisho, ilhali wamemuacha. “Watu wanashindwa kuelewa, mimi silalamiki kuachwa katika hiyo safari, lakini kinachoniumiza mimi kwanini jina langu litangazwe kwamba naondoka wakati naachwa? Kwani kulikuwa na u

Tanzania ikipitisha sheria ya uraia wa nchi mbili nitaiwakilisha Olimpiki 2020

Image
“Endapo Tanzania itafanikiwa kupitisha katiba yake mpya inayosukwa hivi sasa nchini humo mimi nitafurahi kujumuika na ndugu zangu wa damu kuiwakilisha nchi hiyo katika Olimpiki 2020”   “Mimi ni mzaliwa wa Riverside, California, Marekani, kuzaliwa kwamgu hapa kulitokana na baba yangu kuja Marekani kama mwanafunzi 1993 na kwa mapenzi yake akamleta aliyekuwa rafiki wake ambaye ndiye mke wake na ndiye mama yangu hivi sasa” “Alimtafutia nafasi ya kuja kujiendeleza kimasomo na ndipo mimi nikazaliwa na wawili hao kutokana na mazingira hayo, nilipelekwa Tanzania nikiwa na miaka miwili nikakaa kwa miaka mitano na hata shule ya msingi nilianza Arusha ambapo baadaye wazazi wangu waliamua nirudi kupata elimu Marekani” “Marekani ni nchi yangu ya kuzaliwa ila Tanzania ni nchi yangu kiasili (My ancestral home), ninaipenda sana Tanzania na hata ninaposhiriki mashindano ya shule hapa California huwa wenzangu wananiitaga Tanzanian boy” CHANZO: Haya ni maneno yake Sydney Wilhelm Gi