RIADHA HARD TALK 2014: RT yabariki mjadala wa riadha Holili
SHIRIKISHO la Riadha Tanzania (RT), limeimwagia sifa klabu ya Holili Youth Athletics (HYAC) iliyoko Holili, Wilaya ya Rombo mkoani Kilimanjaro kwa kuandaa mjadala wa kujadili changamoto zinazokabili mchezo wa riadha nchini. Mjadala huo utafanyika kesho katika ukumbi wa Moshi Club ulioko pembezoni mwa mji wa Moshi, mkoani Kilimanjaro, ambapo zaidi ya wadau 100 wanatarajiwa kushiriki. Akizungumza na Tanzania Daima kwa njia ya simu, Katibu Mkuu wa RT, Suleiman Nyambui, alisema shirikisho lake limetoa baraka zote kwa klabu hiyo na mjadala huo na kutoa wito kwa wanamichezo wenye nia njema na maendeleo ya riadha kujitokeza kwa wingi kushiriki. Nyambui, aliwataka wadau wa riadha waelewe kwamba mjadala huo haujaandaliwa kwa ajili ya kusutana bali kuunganisha akili kuangalia mbinu za kutatua changamoto zinazokabili michezo hapa nchini. “Watanzania na wapenzi wa riadha waelewe kwamba mjadala huu utalenga kujadili matatizo yetu kama taifa katika riadha na kuangalia mbele, t...