Wilbard Peter na Catherine Lange watwaa ubingwa Karatu Sports Festival
Catherine Lange @ Sokoine Marathon Leo mji mdogo wa Karatu uliopo jirani kabisa na Ngorongoro Crater umeshuhudia mbio za kasi za umbali wa kilomita 10 zilizoshirikisha wanariadha wa Tanzania. Wilbard Peter wa Chuo cha Polisi Moshi (CCP) alishika nafasi ya kwanza akifuatiwa na John Leonard wa Hakika Club na nafasi ya tatu kuchukuliwa na Joseph Theophil wa Guang Club ya Mbulu. Kwa upande wa wanawake mwanariadha mahiri C atherine Lange wa timu ya Magereza Arusha alishinda, nafasi ya pili ikidhibitiwa na Merry Naali wa Ambassador Club na nafasi ya tatu ikienda kwa Angelina Tsere waWSSS. Mtazamo: Kwa mtazamo wa haraka ni kwamba mbio hizo zimefana kuliko mbio zilizokimbiwa hivi karibuni kwa kujali zaidi ushiriki wa wanariadha wazalendo kwa kutozingatia ushiriki wa wanariadha kutoka nje ya Tanzania. Usumbufu unaojitokeza mara nyingi ni pale ambapo MAWAKALA wa wakimbiaji wa nje ya nchi huwa wanafanya UHUNI wa kuwadhulumu wakimbiaji wazalendo kwa kuwapendelea zaidi w...