Posts

Showing posts from March 30, 2014

SOKOINE MINI MARATHON 2014: Usajili wa namba za washiriki umeanza rasmi

Image
Namba zimeanza kutolewa kwa washiriki wa mbio za Sokoine Mini Marathon Km 21 na Km 2 ambazo zitatimua vumbi Aprili 12, 2014 Monduli mkoani Arusha, rais Jakaya Kikwete ndiye atakayepuliza kipenga cha kuanza mbio hizo. Ada ya namba ni Tsh: 2,000 tu, namba zinapatikana Arusha pale Uwanja wa kumbukumbu ya SHEIKH AMRI ABED KARUME na Monduli pia. Kwa washiriki wote nje ya mkoa wa Arusha wasiliana na VICTOR MACHOTA kwa 0787415864 ambaye atapokea usajili kwa njia ya simu na namba yako utajulishwa kwa SMS na itahifadhiwa hadi utakapoichukua. Mwisho wa kuchukua namba yako ni Ijumaa April 11, 2014 Arusha mjini. Kwa wale watakaosajili kwa njia ya simu tunaomba mtume hela kwa AIRTEL MANEY kwa namba ya Victor Machota, unaombwa uongezee gharama kidogo ya kutoa pesa mtandaoni. Kwa wale watakaosajili namba papo kwa papo wawasiliane na PHAUSTIN BAHA 0753860668 kwa maelezo zaidi na kwa wale wa Monduli wawasiliane na ROBERT MOLEL kwa 0753739128. Kwa ratiba kamili hapo baadae pitia

‘Jakaya Kikwete Sports Village’ kujengwa Dom

Image
Mfano wa ramani ya Center inayotarajiwa ya Dr. Jakaya Kikwete National Sports Village MAANDALIZI ya ujenzi wa kijiji cha michezo kitakachojulikana kama Jakaya Kikwete Sports Village yanaendelea vizuri, ambako tayari Ikulu, Baraza la Michezo la Taifa (BMT) na Wizara ya Michezo wametoa baraka kijengwe mjini Dodoma. Akizungumza na   Tanzania Daima , Mratibu wa ujenzi wa kituo hicho, Wilhelm Gidabuday, alisema ujenzi wa kituo hicho kikubwa na cha kwanza nchini, tayari maandalizi yake yameshafikia pazuri na Ikulu ya Tanzania kupitia ofisi ya Katibu wa Rais, imeshawapa baraka ya kutumia jina la Rais katika kituo hicho. Gidabuday alisema, wiki iliyopita walikutana na Katibu wa Rais, ambako waliwasilisha maombi yao na kukubaliwa na kwamba, kuanzia sasa kituo hicho ambacho ujenzi wake utasaidia kuinua vipaji vya michezo yote hapa nchini, kitafahamika kama kituo cha michezo cha Jakaya Kikwete (Jakaya Kikwete Sports Village). “Nidokeze tu kuwa, mipango yote inakwenda sawa, tumeshafikis

OFA: Makampuni yanakaribishwa Sokoine Marathon "Corporate Team Challenge"

Image
Kama njia ya ushirikiano na makampuni ambayo huwa inakuwa mstari wa mbele kudhamini michezo; Tunayo furaha kukaribisha kampuni zenye kutaka kushiriki na kutangaza bidhaa zao. Kwa watakaokidhi masharti wataruhusiwa kuweka HEMA la mauzo na matangazo ya bidhaa zao. Michezo ni kila kitu ikiwemo elimu, afya, ajira, biashara, utalii, diplomasia UZALENDO etc. Karibuni sana watanzania wote.