CECAFA: Kilimanjaro Stars yaibwaga Uganda The Cranes goli 5 kwa 4
Kilimanjaro Stars Timu ya Tanzania ya Kilimanjaro Stars leo imewatoa mashabiki wake kimasomaso kwa kuigaragaza Uganda The Cranes mabao 5 kwa 4 hivi leo mjini Mombasa Kenya. Katika hali ya kushangaza Kilimanjaro Stars waliibuka washindi baada ya mchezo kutawaliwa na waganda katika kipindi cha kwanza ambapo Uganda The Cranes waliongoza kwa bao moja bila kabla ya wabongo kusawazisha na hatimaye kuwapa deni la goli moja pale walipokwenda mapumziko. Katika kipindi cha pili mchezaji wa Kili Stars Salum Abubakar alitolewa kwa kadi nyekundu ambapo waganda walipata mwanya wa kusawazisha bao la pili hadi mwisho wa dakika 90. Ikaja mikwaju ya penati ambapo Kili Stars ilianza kwa kukosa penati mbili mfululizo, lakini waganda nao wakakosa penati mbili kati ya tatu walizopiga, hadi mpira unaisha wabongo walipata penati 3 Cranes wakibahatika na 2 pekee hivyo kuwapa Kilimanjaro Stars ushindi wa jumla ya mabao MATANO kwa MANNE . Awali watanzania wengi walisikika mitaani wakiwa wamek...