Posts

Showing posts from August 31, 2014

Nyambui ataka kung’atuka RT

Image
Katibu wa Chama cha Riadha Tanzania (RT), Suleiman Nyambui amemtaka mtu yeyote anayeweza kuongoza chama hicho ajitokeze ili yeye ang’atuke na kumwachia madaraka. Nyambui alisema katika mahojiano kuwa yuko tayari kujiuzulu wadhifa huo ndani ya RT kama atatokea mtu ambaye anadhani akimwachia cheo hicho ataweza kuleta mafanikio katika mchezo huo. Kigogo huyo wa RT alisema amekuwa akifanyiwa fitina na baadhi ya watu waliowahi kumshawishi kuungana nao ili wapate fursa ya kuitumia RT kufanya maovu yao, lakini walipokumbana na ‘kigingi’ chake wameanza kumfanyia fitina. “Baadhi ya watu wananizungumzia vibaya. Lakini niko tayari kuondoka RT hata leo kama mimi ndiyo kikwazo cha mafanikio ya riadha endapo tu akitokea mtu ambaye atanithibitishia kuwa ana uwezo wa kuleta mafanikio,” alisema Nyambui. CHANZO: Mwananchi

Thadeo calls for fair refereeing

Image
National Director of Sports Leonard Thadeo presents Asma Shafi with a certificate for taking part in a five-day Copa Coca-Cola referees and coaches course at the National Stadium in Dar es Salaam over the weekend. Photo | Michael Matemanga   The National Director of Sports, Leonard Thadeo, has exhorted football referees in the country to observe fair play and abide by the laws of the game while officiating matches at various tournaments. Thadeo made the call during the official closing of a five-day referees and coaches course for the forthcoming U15 Copa Coca-Cola tournament at the National Stadium over the weekend. He said that in recent years there has been an outcry on biased refereeing and challenged the referees to live up to the public expectations of advocating ‘nothing else but fair decisions’. “After all, this is a career you have chosen to earn your living from and we don’t expect you to be lured by gifts or money at the expense of jeopardising your ...

Tufanye sensa ya vyama vya michezo nchini

Image
Dioniz Malinzi / Bosi wa Baraza la Michezo Tanzania Mwaka 2014 unakaribia kumalizika. Ni dhahiri hali ni mbaya katika medani ya michezo nchini na hiyo ni kutokana na matokeo tuliyoona kwa timu na wanamichezo wetu. Kimsingi, Tanzania imeharibu na kutia aibu kuanzia soka, ambayo ndiyo mchezo maarufu, hadi michezo mingine. Viongozi wenye dhamana katika michezo na wao wanaingiza siasa badala ya kuangalia nini wajibu wao na kwa chama na manufaa ya taifa. Tumewahi kupiga kelele sana katika eneo la michezo kuwa udhaifu wa uongozi na hasa kwa kutokuwa na dhamira na dira ya maendeleo, ndiyo kunachangia kutopiga hatua. Kuvurunda kwa wanamichezo wa Tanzania katika mashindano mbalimbali, kutokana na kukosa umakini na zaidi ni udhaifu wa uongozi katika vyama na klabu. Kwa jinsi hiyo, itachukua muda mrefu Tanzania kupiga hatua katika michezo kama mfumo wa utendaji ndani ya vyama hautabadilika. Kutokana na msingi huo, kuna haja kwa mamlaka inayohusika na michezo yote kufany...