Posts

Showing posts from January 19, 2014

MAZISHI: Charles Kyando maarufu kwa jina la Tola kuzikwa siku ya Jumamosi tarehe 25/01/2014

Image
Mazishi ya aliyekuwa kocha wa mchezo wa tenisi Charles Kyando maarufu kwa jina la Tola yatafanyika kesho nyumbani kwake Mwananyamala kwa Ali Maua. Marehemu alifariki usiku wa kuamkia jana baada ya kuugua kwa muda mfupi. Mazishi hayo yatafanyika kesho kwa mujibu wa habari kutoka kwa familia ya marehemu. “Huu ni msiba kwa chama cha Tennis Tanzania na taifa kwa ujumla; pengo lake kamwe halitazibika” alisema kocha wa tenis mwenzake ndg Hassan Kassim. ‘Mwnyezi mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi amina’ Pole nyingi kwa familia, ndugu na marafiki bila kusahau Tanzania Tennis Association .

UTAIFA KWANZA: Mbio za kumbu kumbu ya hayati Edward Moringe Sokoine zitafanyika Monduli mwezi Aprili 12, 2014

Image
Mwaka huu Tanzania inaadhimisha miaka 30 tangu kifo cha aliyekuwa waziri mkuu Hayati Edward Moringe Sokoine .  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dr. Jakaya Kikwete atakuwa mgeni rasmi katika dhifa hiyo itakayofanyika kitaifa Monduli mahali alipozaliwa kiongozi huyo shupavu. Madhumuni ya kuandaa mbio hizo ni kuthamini bidii,   uzalendo na ujasiri aliotuonyesha wakati wa uhai wake. Watanzania wote wanaojali utu, haki, amani na Utaifa Kwanza mnakaribishwa katika kumbu kumbu hiyo. ‘Tujikumbushe baadhi ya nukuu zake akiwa waziri mkuu’   “Ole wake kiongozi mzembe na asiye na nidhamu nitakayemkuta: Kiongozi wa siasa hana usalama wa aina yoyote. Usalama wake ni kudra ya Mungu na Wananchi peke yake. Viongozi wazembe na wabadhirifu wahesabu siku zao. Labda tusiwajue. Hawa hatuna sababu ya kuwapa imani, kuwa tutawalinda kama vitendo vyao viovu” - Edward Moringe Sokoine, 26 Machi 1983. “Katika nchi inayojali haki na usawa, majeshi hayana budi yawe ni chomb

Msiba chama cha Tennis: TTA yapata msiba mzito baada ya kocha wake mkongwe CHARLES KYANDO (TOLA) kufariki ghafla

Image
Charles Kyando (Tola) Enzi za uhai wake Sekta ya michezo Tanzania imepata msiba mkubwa usiku wa kuamkia leo kwa kufiwa na Charles Kyando maarufu kwa jina la Tola , Kyando alifariki ghafla baada ya kuugua kwa muda mfupi. Charles Kyando (Tola) alizaliwa 1968 jijini Dar Es Salaam na wakati wa uhai wake aliwahi kucheza mashindano mbalimbali ya mchezo wa tenisi na kufikia viwango vya kitaifa kati ya miaka ya 1980 hadi 1990. Baada ya kustaafu kama mchezaji bwana Kyando alikuwa kocha wa mchezo wa tenisi na pia alikuwa mtaalam maarufu wa kusuka rakets za mchezo huo. Marehemu ameacha mjane na watoto wawili, pia marehemu ameacha pengo kubwa na isiyozibika katika mchezo wa tenisi na katika chama cha tenisi Tanzania ( Tanzania Tennis Association ). Kuhusu taratibu za mazishi na taarifa zozote kuhusiana na msiba huu tafadhali endelea kusoma blogu hii ya Utaifa Kwanza .

Magunia 16 ya bangi (Marijuana) yakamatwa jijini Arusha baada ya msako mkali

Image
Mkuu wa kitengo cha kuzuia na kupambana na madawa ya kulevya Mkoa wa Arusha Mratibu Msaidizi wa Polisi (ASP) Aben Mgode akiwaonyesha waandishi wa habari misokoto 5000 na magunia 16 ya bangi yaliyokamatwa kufuatia misako mbalimbali iliyofanyika mkoani hapa. Watu saba wakiwemo wanawake wawili wamekamatwa na misokoto 5000  ya madawa ya kulevya aina ya bangi pamoja na mirungi kilo 47. Tukio hilo lilitokea mwishoni mwa wiki iliyopita katika eneo la Mti mmoja lililopo wilaya ya Monduli.