Posts

Showing posts from May 4, 2014

VITUKO: Chama Cha Riadha Tanzania (RT) lawamani

Image
Mwl. Samwel Tupa KOCHA maarufu wa riadha, Samwel Tupa, ameulalamikia uongozi wa Riadha Tanzania (RT), kwa kutumia jina lake kama kocha aliyeondoka na wanariadha waliokwenda nchini New Zealand kwa maandalizi ya mashindano ya Jumuiya ya Madola yanayotarajia kufanyika Glasgow, Scotland, Julai mwaka huu. Akizungumza na Tanzania Daima kwa njia ya simu akiwa jijini Arusha, Tupa alisema hajui sababu iliyofanya uongozi huo kufanya hivyo, na kwamba mara ya mwisho aliwasiliana na Katibu Mkuu wa RT, Suleiman Nyambui, ambaye alimtaka wabaki ili waandae mashindano ya taifa yanayotarajiwa kufanyika Juni. “Nyambui aliponiambia hivyo, nilimwambia mimi kama kocha siwezi nikabaki wakati wanariadha wangu wanakwenda, huko watafundishwa na nani, akadai watakuwa na kocha wa China, lakini mimi sikuafiki hilo na nikajua watakuwa wamebadilisha jina la kocha anayeenda, ila cha kushangaza naona kwenye vyombo vya habari kwamba nimeenda huko,” alisema. Alisema mbali na yeye kuachwa