Posts

Showing posts from August 25, 2013

KATIBA YA RT ILIYO KWAMA NA ATHARI ZAKE: NI JINSI GANI TAIFA LINGEHUJUMIWA; PONGEZI KWA USIKIVU WA BMT NA DEONIZ MALINZI

Image
M/Kiti w BMT Deoniz Malinzi Hivi karibuni viongozi wa Chama Cha Riadha nchini (RT) walijaribu kwa njia zote 'hops and hooks' kupitisha katiba ambayo ingebeba masilahi yao binafsi na siyo masilahi ya taifa la Tanzania. Hata hivyo harakati za wadau wenye taaluma na uzoefu mkubwa wa mchezo wa riadha uliweza kuweka "STOP" katika jitihada hizo zilizovaliwa njuga na baadhi ya viongozi wa RT ambao waliwekwa na TOC na hadi sasa viongozi hao wachache wa juu wa RT bado wanatembelea viatu vya TOC. Deoniz Malinzi: Mwenyekiti wa Baraza la Michezo Tanzania (BMT) alitekeleza wajibu wake vizuri kwa kusikia vilio vya wadau, hatimaye aliangaza macho kupitia rasimu hiyo iliyojaa mbegu za 'ubinafsi' na kuamua kuzuia sheria hiyo isipitishwe hadi marekebisho kadhaa ifanyike. 'Hongera mzee Malinzi' kwa kujali haki na usawa ambao ndiyo chimbuko la amani na ustawi wa jamii na taifa letu la Tanzania. Vipengele vya kijambazi katika rasimu: Mtanzania anayehubiriwa

WIZARA YA MICHEZO INASTAHILI KUWAJIBIKA KWA NANI?; VYAMA VYA MICHEZO AMA TAASISI ISIYO YA KISERIKALI?

Image
FABRIZIO CALDARONE LEONARD THADEO Hivi karibuni Chama Cha Tennis Tanzania (Tanzania Tennis Association) kilipitisha katiba yake na kufanya uchaguzi mkuu wa kuchagua viongozi wake baada ya miaka mingi ya udikteta ndani ya chama hicho. Hata hivyo baada ya muda mfupi wa furaha kwa wapenzi na wadau wa mchezo huo nchini, mzimu wa uongozi wa zamani umeendelea kuikumba taasisi hiyo muhimu katika michezo. Katibu wa zamani (aliyelazimika kujiuzulu ) INGER NJAU na mwenzake FABRIZIO CALDARONE wamekuja na taasisi yao mpya ya ATP TENNIS FOR CHARITY ambapo huko ulaya kuna taasisi inayofahamika kwa jina la TENNIS FOR AFRICA , “ taasisi hizo mbili zenye majina tofauti lakini zenye wanachama haohao ( Inger Njau na Fabrizio Caldarone ) zina harufu ya utata” alisema mjumbe moja ambaye hakupenda jina lake litajwe. “Lakini utata zaidi ni pale ambapo mkurugenzi wa michezo nchini LEONARD THADEO alipowapa kibali cha kuendesha "shughuli za Tennis" kwa viongozi hao wa kigeni na

PONGEZI: WAJUMBE WA (RT) WAKATAA MJADALA WA KATIBA HADI WADAU WOTE WAPATE FURSA YA KUIPITIA; TOFAUTI NA MATAKWA YA VIONGOZI

Image
Wanariadha wa kimataifa wa Tanzania Morogoro Leo Agosti 25, 2013 ilikuwa siku ya kujadiliwa na kupitishwa kwa katiba mpya ya Chama cha Riadha Tanzania (RT), hata hivyo kwa mara ya kwanza viongozi wenye nyuso za kuogopwa na wajumbe kutoka mikoani hawakuamini macho yao pale ambapo walishuhudia upinzani mkali wenye kuambatana na maswali yaliyoenda shule kutoka kwa wajumbe wa mkutano mkuu kutoka mikoa yote ya Tanzania Bara. Mjadala huo mzito ulianza pale ambapo baadhi ya wajumbe walidai kupewa 'hadidu rejea' kabla ya ajenda kuu kuanza, wengine walihoji vyema kabisa kwamba "huu ni mjadala wa katiba mpya au ni mjadala wa mabadiliko ya katiba"?. Mara ghafla viongozi hao wa RT waliozoea kubebwa ba viongozi wa TOC ambao wameegemea pande zote (RT na TOC) kwa uroho wa kimasilahi, walijikuta wakiwa hawana pa kuegemea kutokana na moto mkali kutoka mikoani. Baada ya mabishano yaliyoambatana na 'Cross Examination' RT na ndugu zao TOC hawakuwa na namna nyingine ba