BUNGE LA MICHEZO: "RIADHA HARD TALK 2014 MOSHI FEBRUARY 9 2014"
Domician Genandi Watanzania wameamua kuuvaa ukweli: Holili Youth Athletic Club iliyopo mkoani Kilimanjaro inaandaa mdahalo utakaowashirikisha wanariadha wote, wadau na viongozi wa chama cha riadha. Mkurugenzi wa Holili Youth Athletic Club ndugu Domician Rwezaura Genandi ameileza gidabuday.blogspot.com kwamba ameamua kufanya hivyo ili kutafuta kwa pamoja jinsi ya kulipatia jawabu kiu ya medali ambayo Tanzania inayo kwa muda mrefu. “Ninaimani kwamba wote kwa pamoja tukiongea ukweli, kukosoana na kuelezana ukweli tutapata jawabu mwisho wa mazungumzo ambayo yatratibiwa kwa uwazi na ukweli” alisema mkuu huyo wa HYAC. "Ikiwa Kweli tunapenda mchezo huu wa riadha; haijalishi wewe ni kiongozi, mdau au mwanariadha basi mdahalo huu utaupenda maana sisi HYAC tumeamua kugharimia ukumbi, chakula cha mchana wa siku hiyo na kuwapata waandishi na vyombo vyao vya habari” aliendelea kusema Domician. Utaifa Kwanza blog inawapongeza HYAC kwa wazo hili zuri ambalo RT ingewach...